09.08.2017: MAMA MWENYE TATIZO LA KUPATA CHOO ALIVYOOMBEWA NA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI

Kulia ni mchungaji Noah Lukumay


Shalom..Mama huyu alifika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika maombi ya.....yaliyofanyika siku ya Jumapili 06.08.2017 kwaajili ya kuombewa.Mama huyu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la choo, kwa wiki nzima hajapata choo. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na waumini wa kanisa hili waliweza kumuombea. Wakati wa kuombewa mama huyu aliguswa na nguvu za Mungu na akajikuta anaanguka chini bila ya kuguswa. Yupo Mungu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akimuombea

Yawezekana na una tatizo la kupata choo kwa muda mrefu, nataka nikwambie kuwa Yesu anaweza kukuponya. Karibu Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni



Comments