30.07.2017: FURAHA YATANDA KATIKA IBADA YA "KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU" ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya siku ya Jumapili 30.07.2017 katika ibada ya "KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwaklatare. Mungu alionekana kugusa maisha ya watu katika kipindi cha kusifu na kuabudu kilichoongozwa na Martha Komanaya na Praise & Worship Team ya hapo kanisani. Nyimbo zao zilifanyika baraka mbele za Mungu na mbele za watu wake. Watu walionekana kuguswa na ujumbe mzito uliokuwa ukitolewa na watumishi wa Mungu kupitia nyimbo zao. 

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuungana na waumini wa kanisa hilo na kwa kuimba na kumsifu Mungu. Ibada ilizungukwa na uwepo wa Mungu. Hakika Mungu wa Mlima wa Moto ni Mungu wa kuheshimika kutokana na mambo makuu anayofanya kupitia kipindi cha sifa. Miyo ya watu inahuishwa upya, watu wanapata nguvu ya kusikiliza Neno, watu wanaondolewa na usongo wa mawazo, watu wanaponywa, watu wanapata matuamini ya mafanikio, watu wanainuliwa imani zao. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Martha Komanya


 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare











Comments