23.07.2017: MATUKIO KATIKA PICHA ZA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIKIHUBIRI SIKU YA JUMAPILI

Hivi ndivyo tulivyomuona Mungu akishungulika na maisha ya watu katika ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada ilikuwa na upako wa ajabu sana, watu walibarikiwa na mahubiri kutoka kwa Mh. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji waliokuwepo siku hiyo. Tukiwa tupo katika maadalizi ya mahubiri ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" tunawapongeza na kuwaombea wageni wote waliofika katika ibada hii pamoja na wale waliamua kujiunga rasmi na kanisa hili na wale wote walioamua kuokoka na kubatizwa kkwa maji mengi.

Ibada hii ilikuwa na uwepo Mungu kila mahali, tuliona Mungu akitufariji na kututia moyo kupitia mtumishi wake Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji wa kanisa la Milma wa Moto Mikocheni "B". Hakika watu tulitoka tukiwa watu wa tofauti sana na tulipooingia ibada, ile hali ya kuona tu wapweke ilitoweka, hali ya kuwa na machungu yalitoweka, hofu na mashaka vilitoka, wenye magonjwa mbalimbali wengine walipona na wengine waliondolewa maumivu yao, wenye uhitaji wowote ule, Mungu alionyesha njia pasipo na njia za watu kufikia malengo yao.

Inawezekana unatamani kufika kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" na hujui ibada inaanza lini na saa ngapi? Sasa, ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...





































Comments