23.07.2017: WANANDOA WAMSHUKURU MUNGU NA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWEAKATARE KUFANIKISHA HARUSI YAO

Wanandoa hawa siku ya Jumapili 23.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwenye ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU YETU waliweza kumshukuru Mungu kwa kuwafanikisha maandalizi ya harusi yao na siku ya harusi yao, walimshukuru Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi yake tangia walipoanza uchumba mpaka siku ya harusi, walimshukuru Mch. Noah Lukumay kwa mafundisho ya ndoa, waliwashukuru wazee wa kanisani, wachungaji, vijana, wainjilisti, wahudumu na waumini wote wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa jinsi walivyojitoa kufanikisha harusi yao. walisema, waliona mkono wa Mungu katikakipindi chote cha maandalizi yao ya harusi na mapaka sasa wako kwenye ndoa.

Wazazi wa wanandoa hao walimshukuru sana Mungu pamoja na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa upendo alioonyesha kwa watoto wao. walisema Bishop alichukua nafasi kama mzazi kuhakikisha ndoa inafungwa kwa amani.

Yawezekana umetafuta sana mchumba au mahusiano yenu hayako sawa au umeachika na mpenzi wako, nataka nikuambie Yesu anaweza kurudisha mahusiano yenu, uchumba wenu, unachotakiwa ni kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu, kuomba na kufunga, kukemea roho chafu, kushiriki ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B", kusikiliza Roho Mtakatifu, kutii kile ambacho mwezako anakuambia kama ni chema, punguza kiburi na majivuno, acha tabia mbaya, usiwe muongo kwa mwezako, muwe na uhakika wa mahusiano yenu, muwe watoaji kanisani, na kufanya yaliyomema mbele za Mungu bila ya kusahau kutubu thambi zenu kila wakati.

Tunakukaribisha katika Ibada ya Jumapili hii itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana
Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...


 









Comments