23.07.2017: MC. JOSHUA MAKONDEKO AGUSA MIOYO YA WATU KWA NYIMBO YAKE SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mungu azidi kumlinda na kumtunza mtumishi wa Mungu Mc. Joshua Makondeko kwa kazi nzito anayofanya ya kumtumikia Mungu. Siku ya Jumapili 23.07.2017 amefanyika baraka sana katika ibada ya KUKOMESHA MAUMIVU iliyofanyika katika kanisa la Mungu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.. Watumishi wa Mungu walicheza na kufurahi wimbo wake wa TUTAPITA KATIKATI YAO. Wimbo huu umekuwa na mafuta ya upako kwa mzee, kijana na hata mtoto, ni wimbo ambao umekubalika na jamii kutokana na ujumbe mzito na upako wa kipekee. Yawezekana hujabahatika kuusikia, ingia YOUTUBE na utabarikiwa sana.

Mungu ambariki sana mtumishi huyu wa Mungu pamoja na familia yake. Amen

Nikukaribishe wewe ambaye hukuweza kufika kanisani siku ya Jumapili. Ibada ya Jumapili hii itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...













Comments