23.07.2017: BAADHI YA WAZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAKIOMBEWA NA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na jopo la wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" pamoja na kanisa zima siku ya Jumapili 23.07.2017 waliweza kuwaombea wazee wa kanisa. 

Pengine na wewe unahitaji kuombewa katika biashara yako, ajira yako, kazi yako, masomo yako, mahusiano yenu, promosheni, kibali katika kila jambo unalofanya, maendeleo yako, afya yako n.k basi usikose kushiriki ibada za Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katika ya wiki kuanzia saa 9 alasiri. Ukifika hapa utakutana na watumishi wa Mungu nao watakuombea kulingana na hitaji lako. Mungu wa HAKI ataingilia kati kutatua shida yako. Watu wengi sana wamefika katika kanisa hili kwaajili ya kuombewa na Mungu ameweza kujibu maombi yao na sasa wanafurahia NEEMA ya BWANA. Tunajivunia na Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwasababu anajibu kila tuombalo.

Hapa yupo Mungu anayeponya kansa, UKIMWI, vidonda sugu, TB,Pressure, Kisukari, matumbo, maumivu ya mgongo na viuno, kichwa na magonjwa mbalimbali. Pia ni Mungu anayeinua watu kutoka ZERO na kuwa matajiri, ni Mungu anaiyefariji unapopitia magumu, ni Mungu anayetusaidia kupata mafanikio, kibali, promosheni, afya njema, k ulinzi n.k.

Unapoona unapitia changamoto basi mtazame Mungu juu naye atakusaidia kwani ametusaidia wengiu katika maisha yetu. Tunakukaribisha Jumapili hii kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa barabara ya Coca Cola...

















Comments