16.07.2017: WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAKIPELEKA MASHITAKA KWA MUNGU DHIDI YA MAADUI WANAOWATAKIA MABAYA

Katika maisha yetu ya kumtegemea Mungu unapoona umeanza kupitia changamoto kali unatakiwa kumuangalia Mungu pekee na KUMPELEKA MASHITAKA YAKO KWAKE kwa yale unayopitia ili akusaidie uwe katika mikono salama kimwili na kiroho. Watu wengi sana katika Biblia walipopitia magumu walimtegemea Mungu na kumuomba awasaidie kuwavusha pale walipokwama.

Siku ya Jumapili 16.07.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Bishop Gertrude Rwakatare alipata ufunuo wa kuandaa ibada maalum ya KUPELEKA MASHITAKA YETU KWA MUNGU. Watu waliweza kuandika vile ambavyo walitaka Mungu awatendee. Kuna watu wanapitia changamoto mbalimbali kama vile uhakika wa kupata chakula, njaa, umaskini, magonjwa, kukosa kazi, kukosa ajairia, kulogwa, roho chafu, kufeli masomo, kunenewa maneno mbaya ya kutofanikiwa, kujiua, umalaya, umbeya, kuua, madeni, njaa ndani ya myumba, na mengine kama hayo; watu hawa wanahitaji kuona mkono wa Mungu ukiwashika na kuwavikisha mahali palipo salama. Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba mkono wa BWANA umeshanyooshwa kwako , unahitaji kujitakasa na kuushika mkono huu wa huruma ili Mungu akuvute hapo ulipo na kwenda mahali pa baraka tele. Endelea kumtafuta BWANA naye hata urudisha mkono wake nyuma mpaka umemshika.

Mungu anakupenda sana na ndio maana amekuwa akikutetea na kukupa afya njema, na kama wewe unaumwa au unapitia mapito magumu lakini bado Mungu anakupenda na ndio maana bado unaishi.

Watumishi wa Mungu wamekuwa wakikuagiza kuja na vita fulani ili viombewe; Wengi wao wamepokea miujiza yao baada ya kutii sauti ya Mungu kupitia vinywa vya watumishi wake waliopo hapa duniani..

Katika ibada ya maombi ya kupeleka mashitaka yetu kwa Mungu, watu waliandika mahitaji yao na vitu vinavyowasumbua katika maisha yao na waliweza kuyaweka mahitaji yao walioandika katika madhababu. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliomba pamoja wa na kanisa zima. Na hivi sasa watu wameanza kupokea miuijiza yao. Natumaini unatamaini Upako Huu wa Aina Yake, jiunganishe na mtandao wa Yesu Kristo kwa kufika katika ibada za Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana









































































Comments