16.07.2017: ANGALI PICHA HIZI AMBAZO ZINAOONYESHA JINSI YESU ALIVYOKUWA AKIGUSA SHIDA ZA WATU SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 16.07.2017 katika semina ya MID YEAR CROSS OVER 2017 iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Bishop Dunstan Maboya aliweza kuwaombea watu wenye shida mbalimbali na wengi wao waliweza kupokea miuijiza yao hapo kwa hapo na kukiri kwa vinywa vyao kuwa wamepokea yale waliyokuwa wakiyaomba.

Hakika Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" anajibu kwa moto. Unachotakiwa ni kuwa mwaminifu mble za Mungu, kufuata taratibu zake anazotuagiza kupitia kitabi chake kitakatifu yaani Biblia, kuwapenda watu wote kama unavyojipenda, kuwa mtoaji kanisani, kusaidia wenye uhitaji, kutenda yaliyo mema kwa kila mtu.

Yawezekana na wewe ungetamani kuona mkono wa Mungu juu ya maisha yako, unatamani kuona Mungu anakuvusha katika jaribu lako, anakuvusha katika biashara yako n.k, karibu Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, utakutana na nguvu za Mungu kupitia watumishi wake. Mungu na akubariki sana.



























Comments