28.05.2017: MCH. NOAH LUKUMAY: JENGA MSINGI WA MAISHA YAKO JUU YA MWABA IMARA

Mch. Noah Lukumay wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 28.05.2017 alikuwa na haya ya kusema, Bwana Yesu asifiwe, Maandiko yanasema “Mahali palipo Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru.” Katika Biblia Daudi anasema, “Asizimie mtu moyo”, mwambie jirani yako, “Jenga msingi juu ya mwamba”. Ukisoma Yoshua 1:7 inasema, “Uwe na uhodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu, usiache kwenda mkono wa kuume au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.” Msingi wako wa mafanikio yako uko ndani ya Neno. Je, msingi wa imani yako uko wapi? Ushindi wa kila mtu uko katika Neno la Mungu. Ukikuta mtu anaomba bila Neno ataishia kusema, vitu ambavyo havieleweki, lakini ukiona mtu ambaye anaomba, na anasoma Neno basi matokeo yake utayaona yakiwa mazuri, mtu huyo anakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji uenezao mizizi yake kila kona. Sasa, sema, Ee Bwana Yesu nahitaji kusoma Neno nakuomba. Hatua ya ushindi wa kila mtu uko kwenye maombi na Neno. Ukisoma Luka 4:1 Maandiko yanasema, “Roho Mtakatifu akampandisha Yesu mlimani kwenda kuomba siku 40, na alipokuwa akiomba shetani akamwambia, ”Wewe si mwana wa Mungu badilisha mawe kuwa mkate”, Yesu hakumjibu kwa kusema, “Kwa jina la Yesu toka”, hakumwambia “Pepo mchafu ondoka”, alimwambia, ”Imeandikwa.” Shetani akikujilia hata kama anakuonyesha matatizo mwambie, anakwambi mpaka leo haujaolewa, hujajenga nyumba, hujapata kazi
mwambie “Imeandikwa mtu hata ishi kwa kila viti alivyonavyo bali kwa kila Neno litokalo kwenye kinywa cha Bwana. Unajua tukitaka kutengeneza ma-”champion” lazima wawepo watu wanaopenda Neno la Mungu, lakini tukiwatengeneza watu wanaokula pelemende na pipi na chocolate, tutawatengeneza watu buibui ambao hawataweza safari ndefu iliyopo mbele yetu.
Katika safari ngumu unayoendea, kuna watu watasema, “Wewe hufai” lakini wewe sema, “Mimi najua niliyemfuata na sio mwanadamu.” Katika Biblia Yoshua anasema, “Hili Neno lisiondoke kinywani mwako bali uyatafakari mchana na usiku.” Ukisoma Waebrania 11:3 Maandiko yanasema, “Vitu vyote vimeubwa kwa Neno wala hakuna jambo ambalo lipo lakini kila jambo limefanywa kwa Neno la Mungu.” Kile unacho kihitaji kinategemeana sana ndani yako. Acha na maneno ya watu hayatakufikisha mbali. Watu wengi wanasikiliza maneno ya watu ambayo yanakwaza, yanaumiza, yanavunja moyo, wanaacha kusikiliza hii sheria. Ukisoma Mathayo 8: 5 inasema, Yule mkuu alimwambia Yesu, “Kunashida nyumbani mwangu, kuna mtu anaumwa”, Yesu akamwambia, “Wacha twende nyumbani kwako”, akamwambia, “Hapana kwangu mimi sikuhitaji, najua mamlaka uliyo nayo, mamlaka yako ni ya kusema neno, sasa sema neno tu na mtumishi wangu atapona”, Yesu akamwambia, “Katika nchi ya Yelusalem sijawasi kusikia mtu mwenye imani kama hii kwa nini hatafuti vitu vinavyoonekana, anatafuta nguvu ya Neno.” Mwambie jirani yako kuna nguvu ndani ya Neno, watu wengi tunaongea lakini tuko kinyume na lile Neno Mungu analolisema, na hii kwa sababu hatuko na line Neno la Mungu. “Kimjaacho mtu ndani ndicho kitokacho nje”, unachokiongea ni kile amacho kipo ndani yako ndio maana kila wakati umejaa kushindwa, kukata tamaa, vitu vingi vinakutesa kwa sababu ile sheria ya Mungu haimo ndani yako ile sheria ya kushinda vipingamizi haipo ndani yako, ile sheria ya kupata nguvu ya Mungu haipo ndani yako. Inua mkono wako juu sema kwa jina la Yesu siku ya leo, sheria ya Bwana ikawe sehemu ya maisha yangu Ee Bwana Yesu simama nami katika jina la yesu.

Lazima ujue kutumia nguvu iliyopo kwenye Neno, usipo itambua utakuwa ni mtu unayeishi na matatizo, utakuwa mkristo bandia ambaye hueleweki unaenda wapi kwa sababu hauna nguvu ya Neno la Mungu ndani yako. Sema, “Ee Bwana Yesu, nguvu ya Neno lako iwe sehemu ya maisha yangu.” Ukisoma Yeremia 1:9 neno linasema, “Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake akanigusa kinywa changu, Bwana akaniambia, Tazama nimetia maneno yangu kinywani mwako, angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme ili kung’oa na kubomoa na kuharibu na kuangamiza ili kujenga na kupanda. Mstari wa 19 unasema, ”Nao watapigana nawe lakini hawatakushinda, maana mimi nipo pamoja nawe asema Bwana ili nikuokoe.” Unapokuwa na Neno la BWANA lazima usimame kuokoa na kubomoa alafu unasema kwamba, “maana Mungu atakuwa na mimi”, yaani lile Neno ni king’amuzi, ni msumali inayosababisha vitu unavyovihitaji viwepo ndani yako, unapoomba hauna haja ya kubabaika maana tayari Neno limejaa kwenye kinywa chako, kwahiyo wewe ukikaa kwa Yesu na maneno yake yakiwa ndani yako tayari kila unachokihitaji kipo. Shetani anachokitaka ni kuinuka juu ya mtu wa Mungu ili akutumikishe, akiinuka juu ya ile elimu unayojua kuhusu Mungu. Shetani akiwa juu yako tu akisema kwani Mungu alisema hivi kwa sababu ipi? Hapohapo ashakubadilishia amekunyang’anya dhahabu original, ameshakupa dhahabu “fake.” Na wengi wao wametekwa na shetani kwa sababu kwenye akili shetani ndio mtu asiyemjua Mungu anakuwepo , anamtoa ufahamu. Unatakiwa kujua kuwa imani yetu haiji kwa sababu nyingine ni kwa kusikia Neno la Bwana. Ukitaka kuinuka kimaisha sikiliza sana Neno la Mungu. Watu wengi wamesikiliza sana umbeya wamebaki kuwa watu wa mtaani.

Mch. Noah Lukumay







Mch. Stanley Nnko




































xxx
















































Comments