11.06.2017: UJUMBE: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ASISITIZA WATU KUWA NA UPENDO


Mungu wetu ni Mungu wa UPENDO. Anatupenda bila gharama yoyote ile. Sasa na wewe onyesha upendo kwa kila mtu bila kuchagua rangi, dini, kabila, tabaka wala hali yao ya kiuchumi. Kuwepo leo ni kwa neema ya Mungu, kuna watu waliatamini kuwepo lakini haikuwezekana - huu ni upendo wa ajabu sana.

Yesu Kristo alitupenda sisi sote bila ya kuangalia imani ya mtu wala rangi ya mtu zetu wala rangi zetu. Alikuja duniani kwa wema na wabaya. Alivumilia maovu yetu....

Siku ya leo tamani kuonyesha upendo kwa kila mtu kwa kumpa zawadi, kumsalimia, kumjali, kumtembelea, kumtia moyo, kumfariji n.k

Nikupongeze wewe uliyeonyesha upendo wako siku ya Jumapili 11.06.2017 kwa kufika kanisani na kuabudu nasi Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kushiriki ibada ya NEEMA YA KUANZA UPYA. Mungu akusaidie uanze maisha yako upya na yaliyojaa amani na furaha.

/ /SASA NAOMBA U-SHARE, LIKE NA COMMENT kwa UTUKUFU wa BWANA.//
//Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada zetu siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana//
//Facebook: Mountainoffire Tanzania au Bishop Gertrude Rwakatare //
//Youtube andika Mlima wa Moto au Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu na watu wakisema kanisa kwa Mamam Rwakatare..Ingia humo//

Comments