11.06.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWATAKA WATU KUWAHESHIMU WATUMISHI WA MUNGU KWANI WAMEBEBA BARAKA ZAO KATIKA IBADA YA "NEEMA YA KUANZA UPAYA"

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alikuwa na haya ya kusema katika ibada ya Jumapili Bwana Yesu asifiwe. Katika  ibada ya Jumapili 11.06.2017  ya NEEMA YA KUANZA MPYA (The Grace To Start Again), alisema. Bwana Yesu apewe sifa,  nataka tujifunze kitu juu ya NEEMA YA KUANZA UPYA. Unajua, NEEMA ni kitu cha UPENDELEO kutoka kwa Mungu. Ninaomba kwa Mungu huu UPENDELEO wa Mungu ukushukie leo. Unaweza kuwa umekwama katika lolote lile, lakini leo ni siku yako ya Mungu kuondoa lile lillokushinda na kuingiza jipya. Leo Mungu atakutendea jambo jipya, atakarabati maisha yako kuwa mapya, afya yako kuwa mpya, uchumi wako na kuwa na fedha mkononi.

watu wengĂ© wamekwama, wamegoti, hawajui pa kuingilia wala kutokea. Sasa katika kukwama kuna mambo mengi yanayosababisha watu kukwama, lakini mimi siku ya leo naona ni vizuri niwape nuru, niwape mwanga, niwape nja ili ukitoka hapo usikwame tena. 

Leo ninataka nikufundishe FAIDA MUHIMU ZA KUWAHESHIMU WATUMISHI WA MUNGU WALIO MBELE YAKO.
Unaweza kuona wachungaji wapo mbele ya madhabahu na kuanza kusema, "Unajua mama wa Kipogolo bwana, kimama chenyewe kifupi, siku hizi ni kizee hakiweze kuhubiri.". Mimi nataka kukuambia kwamba kupiti huyo mchungaji kuna baraka zako. Kama Mungu ameniweka mbele, basi nina baraka zako ili nikufikishe mahali fulani.

"Kwa mkono wa Nabii Israel ilitolewa Misri ikaingizwa Kanani na ilihifadhiwa jangwani. Walimuamini Musa hata kama alikuwa na kigugumizi hawezi kusema. Walipofika bahari wakaanza kumuliza Musa tutafukaje na mbele yetu kuna bahari. Musa akaongea na Mungu wake amuwezeshe kuvuka. Mungu akasema achukue fimbo apige bahari na maji yakagawanyika. Wamisri walipoona wenzao wamepita, wakasema kumbe ni rahisi, nao wakaingia na farasi zao, na meli zao, walipofika katikati ya bahari Wamisri wakamezwa na bahari na wote wakafa” Kila unachotaka kwa Mungu kipo mikononi mwa mtumishi wa Mungu aliye mbele yako. Mheshimu upate Baraka na usipofanya hivyo kuna madhara. Kama humwamini mchungaji wako, basi ondoka kwenye kanisa hilo, na kama unamwamini basi mheshimu na kumwamini."

Soma Waefeso 6:1. Unatakiwa kuwatii wazazi wako. Ninaomba usichangaye wazazi wa kimwili na wazazi katika BWANA. Wazazi katika BWANA ni wale wanaosimama mbele yako na wakakufundisha Neno la Mungu. Ila wazazi wa kimwili unatakiwa kuwaheshimu nao ili upate miaka mingi ya kuishi duniani kwasababu wao wamekuzaa na wamekulea.

Kuna baadhi ya wazazi wa kimwili wakishindwa kuongea na watoto wao huwapeleka kanisani kwa wachungaji ili wamuombea na kuwafundisha Neno la Mungu ili liwajenge na kuwa na tabia njema.

Soma Hesabu 12:5.9 na 11. ACHA MASENGENYO. Unatakiwa kujua kuwa hawa wachungaji sio malaika bali ni watu, kwahiyo kuna wakati anaweza akakasirika. Acha tabia ya kuwapachikia majina mabaya wachungaji wako kutokana na udhaifu wao. Jitahidi kujizuia kusema maneno mabaya kwa wachungaji.

Nataka nikuambie ndugu yangu yakuwa hata hayo mateso yako, yawezekana hujalogwa wala hujafungwa ila hauna maelewano na “your original Pastor”. Kumbuka ulifanya nini kwa mchungaji wako, “Go back and repent”. Ukienda kwa mchungaji wako na kutubu makosa yako uliyomkosea, basi ukirudi utakuwa mpya.

Baraka zako ziko kwa mama yako wa Kiroho. Kama mama/baba yako wa kukuzaa anaweza kukutamkia Baraka zako zikatokea basi hata mama/baba yako wa Kiroho anaweza kukutamkia Baraka zako na zikatokea. Nataka ni kwambie  kuwa laana ya wazazi ni mbaya sana. Kwahiyo unatakiwa kujua kuwa kama mzazi wako wa kimwili ana nguvu basi Yule wa kiroho  ana nguvu mara mbili.

Mchungaji wako unatakiwa kumuombea, kumsaidia au kuongea naye ana kwa ana. Usipende kupeleka maneno machafu kuhusu mchungaji wako kwa watu wako na ukaonekana wewe kama vile CNN au BBC. Namuomba sana Mungu akuhurumie.

Unaweza kuona mambo yako hayaendi, kumbe sababu mojawapo ni maneno yako ya kuwachafua wachungaji wako. Jitenge sana na watu wanaowasema watu wengine (Wasengenyaji), wakimbie kwani hao si marafiki ni maadui zako, wanakuangamiza.

Unatakiwa kumheshimu mchungaji wako, kwani Mungu amemuita kwa kazi yake kwahiyo amebeba Baraka zako.

Sio kila magonjwa yanatoka kwa shetani, ila magonjwa mengine yanatokana na jinsi Mungu anavyochukia matendo yako mabaya. Magonjwa mengine Mungu anaruhusu ili wewe ushuke (uachane na tabia zako mbaya).

Leo kuna NEEMA YA KUANZA UPYA, basi anza upya kwa kuwaheshimu watumishi wa Mungu. 

Kuna watu wengine wanaleta sifa mbaya kwa jina lao la UCHUNGAJI. Hata mimi huwa najisikia vibaya sana kujiita mchungaji nikiona mwingine anafanya vibaya. Yesu alisema, "Basi kama hamniamini mimi basi aminini hata kazi zangu." Kazi ninazozifanya basi ziwape IMANI ya kuniamini.

Ninawaomba sana msilizumbue kanisa kwani kanisa linahitaji kuwa tulivu. Wewe umekunywa maji masafi halafu unaanza kuchafua ili wenzako wasinywe!!

Soma Mwanzo 9:18-28

MAHUBIRI YANAENDELEA...ENDELEA KUFUATILIA MAHUBIRI HAYA....





















































Comments