11.06.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWATAKA WATU KUWA NA UPENDO

//Iheshimu sana huduma aliyokupa Mungu//
//Mshukuru Mungu kwa huduma aliyokupa//
//Unavyobarikiwa, wabariki na wengine//
//Kuwa karibu na jamii yako inayokuzunguka//
//Onyesha upendo kwa ndugu na jamaa zako//
//Jishushe na usijione wewe ni bora kuliko wenzako//
//Furahi na wenye furaha, lia na wenye kulia//
//// Nikupongeze wewe uliyeabudu nasi katika ibada ya Jumapili 11.06.2017 Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ule ujumbe uliopata kutoka kwa Mungu kupitia mtumishi wako unaosema "NEEMA YA KUANZA UPYA" ukatimie katika maisha yako. Maisha yako yakabadilike mwezi huu na kuwa bora zaidi kuliko miezi iliyopita. Kama ulikuwa katika nyumba za kupanga ukapate nyumba yako, kama uliajiriwa ukapate ofisi yako, kama hukuolewa wala kuoa ukaoe/kuolewa, kama ulikuwa huna mtoto ukapate mtoto, kama ulikuwa huna gari ukapate gari, kama ulikuwa tasa ukazae watoto wazuri na wenye akili, kama ulikuwa unafeli masomo ukafauli, kama ulikuwa unalogwa na kuteswa ukafunguliwe na wabaya wako yakawapate mabaya mara mia waliyokutendea mpaka watakapookoka, kama huduma yako iliyumba ikashamiri sasa, kama ulichukiwa ukapendwe, kama ulikuwa mtu wa kukopa ukakopeshe, kama biashara yako iliyumba ikashamiri sasa, kama ulikosa kusoma Meno la MUngu ukapate hamu ya kulisoma Neno la Mungu, kama ulikuwa muovu ukatende mema mpaka waliokudharau kwa uovu wako wakashangae, kama uchumi wako ulikuwa hafifu ukaongezeke kwa UKUBWA mpaka watu waachame midomo yao...POKEA BARAKA hizi kwa jina la Yesu Kristo. ///

//SASA NAOMBA U-SHARE, LIKE NA COMMENT kwa UTUKUFU wa BWANA.//

//Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare//
//Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Ibada zetu siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana//

//Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com//
//Facebook: Mountainoffire Tanzania au Bishop Gertrude Rwakatare //
//Youtube andika Mlima wa Moto au Mlima wa Moto Mikocheni "B"//
//Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola utaona magari yetu na watu wakisema kanisa kwa Mamam Rwakatare..Ingia humo//



Comments