14.05.2017: MWENYEKITI WA WAMAMA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AHIMZA WAMAMA KUWAJIAMINI NA KUWAPENDA WAUME ZAO


Mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 14.05.2017 ya MOTHER’S DAY alikuwa na haya ya kusema.Bwana asifiwe, Nachotaka kusema ni kwamba watu wengine wanaona aibu kukuwakumbatia wake zao au waume zao, jamani huyo si ni mke wako, si ni mumeo, si ulimchagua? hebu muone mkeo au mumeo ni mpya kila iitwapo leo. Naomba niwapongeze akina mama kwa kuumbwa mwanamke yaani unastahili. Ukiangalia nyumba yenye amani na upendo, ndipo ambapo Mungu yupo ndani yao, na kila wanalolipanga linapata kibali mbele za Mungu kwasababu ipo amani ndani ya nyumba. Ukisoma Matendo 9, Dorkasi upendo wake ulikuwa unamfanya ashone nguo awape wajane. Mwanamke ndio msingi katika nyumba yake. Utakapoingia katika nyumba ya mwanamke. Ukikuta mambo hayaendi sawa watu wanaanza kusema huyo si mwanamume amefanya ila ni mwanamke kafanya. Waanaume wanatuendesha sana. Unajua penye mafanikio ya mwanaume wanamke yupo nyuma yake. wakienda tofauti hawataona Baraka za Mungu. Mithali inasema, “mwanamke ndio anatafuta.” Mwanamke nyenyuka katafute maendeleo, shirikiana na wenzako usikae peke yako utajifunza mengi, utaona jinsi unavyo badilika utajua jinsi ya kushirikiana na mume wako, kuongea na mume wako, kupanga na mume wako. Mawasiliano yakiwa mazuri yaani kila kitu ndani ya nyumba kitaenda sawa. Kuna akina mama wengine ni “hard working” vibaya muno, mpaka unauliza, hivi huyu ni mwanamke au mwanaume anayefanya hivi vitu vikubwa?. Mahusiano yangu na mume wangu watu huwa wanasema, “umemshika mwanaume kwaajili ya madawa” Jamani hakuna dawa ila angalia mwanaume anapenda nini, anataka nini. Mimi Kuna dada mmoja ananiambia, “Mimi simuelewi mume wangu kila nikitaka kufanya hiki haiwezekani.” Nikishangaa, wewe humuelewi mumeko nani atamuelewa kama sio wewe? Wewe ndo unatakiwa umuelewe mume wako. Mungu awabariki.

Comments