23.04.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIPOKEA ZAWADI KUTOKA KWA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI EPHRAIM EZEKIEL

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Ephraim Ezekiel siku ya Jumapili 23.04.2017 aliweza kumpa zawadi ya kitenge Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare mbele ya madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kutokana na kumkubali katika huduma yake na juhudi zake katika jamii ya Watanzania. 

Baada ya kutoa zawadi hiyo mtumishi wa Mungu Ephraim Ezekiel aliweza kupata muda ya kumuimbia Mungu wetu. Wimbo wake uligusa sana mioyo ya watu na kusababisha watu kutojizuia kucheza. Nyimbo zake zimejaa upako na unapozisikiliza unaona uwepo wa Mungu eneo uliopo. Mungu azidi kumuinua zaidi.Na pia tujaribu kumuunga mkono kwa kununua kazi zake na kumuombea.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akipokea zawadi kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Ephraim Ezekiel











Comments