23.04.2017: MCH. NOAH LUKUMAY WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AWAOMBA WATU KUWA NA UMOJA NDANI YA KANISA NA MSHIKAMANO

Bwana ni mwema, tunaona jinsi anavyozidi kufanya matendo makuu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kila kuitwapo leo. Siku ya Jumapili 23.04.2017 ilikuwa ni siku ya baraka sana kwa wale waliobahatika kufika katika ibada hii. Mungu alionekana akishughulika na maisha ya watu kupitia watumishi wake. Hakika Mungu wa Mlima wa Moto anaonekana kwa walio wake.

Mch. Noah Lukumay aliweza kutubariki sana na Neno la Mungu ambalo hivi karibuni tutalipost hapa kwenye ukurasa na pia video itawekwa YOUTUBE kwaajili yako kuiangalia na kujifunza. Mungu aliweza kuachilia upako wake na kumtumia Mch. Noah Lukumay na kusababisha waumini kuambukizwa ule upako.

Ibada hii ilihudhuriwa na watu wengi sana kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la dar es Salaam, mikoani na nje ya Tanzania. Hii inatokana na yale matunda wanayopata kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake aliowapaka mafuta.

Watu wenye shida mbalimbali kama vile kukosa mume/mke, watoto, kazi, kibali, mafanikio, na mengine kama hayo wamekuwa wakishuhudia jinsi Mungu alivyowainua na kuwabariki baada ya kukaa chini na kufundishwa kutoka kwa watumishi wa Mungu.

Tuna kila sababu ya kukupongeza na kukushukuru wewe uliyebahatika kufika katika ibada hii na kupokea zile baraka za Mungu alizokuahidia kupitia watumishi wake. Na ninaamini na Jumapili hii utakuja kuchochea baraka zako na kuchota baraka zingine kutoka kwa Mungu. Jitihada zako za kumtafuta Mungu kwa bidii ndizo zitakazosababisha wewe kubarikiwa.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mcaha hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Zipo baraka zako kwani watu wengi wanashuhudia jinsi Mungu anavyowatenda baada ya kushiriki ibada zetu na kuyashika yale wanayofundishwa na kuhubiriwa kutoka kwa watumishi wa Mungu. Mungu akubarikisana.

Mch. Noah Lukumay


















































































xxx
















Comments