19.03.2017:WATU WAZIDI KUBATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KAMA ILIVYOTOKEA JUMAPILI ILIYOPITA

Baada ya waumini wapya kuongozwa sala ya TOBA na Mch. Rosemary Mgetha wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waumini hawa walipelekwa baharini kwaajili ya kubatizwa kwa maji mengi. Na walipofika huko walianza kwa kumsifu Mungu, kumwabudu Mungu, kufanya maombezi na baadae kubatizwa. Baada ya kubatizwa waliweza kuombewa na watumishi wa Mungu, na wengi wao walijazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha. Na baadhi yao waliuiweza kutokwa na mapepo, majini na nguvu za giza kwani walionekana kupiga kelele na kungaragara chini huku wakilalamika kuunguzwa na moto.

Siku ya Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu  katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Sasa mimi na wewe tunahitaji kuwaombea hawa ndugu zetu wazidi kusonga mbele kwa kazi ya BWANA na wasirudi nyuma. Hivi sasa shetaniu anawanyemelea ili awaangushe katika wokovu wao, lakini tukismama katika maombi shetani hata weza kamwe. Na wewe uliyeokoka na kubatizwa, anza kuishi maisha matakatifu kwa kujitakaza na kufanya toba kila wakati, soma Neno la Mungu na liishi ndani yako, usikose ibada  kila kuitwapo leo. Ukifanya hayo yote na mengine ambayo ni mema mbele za Mungu utaona milango ya mafanikio ikifunguka katika maisha yako, vifungo vya mateso k=vikikatika. Mungu akubariki sana na karibu katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi 8 mchana Mlima wa Moto Mikocheni"B"







































Comments