MCH. NOAH LUKUMAY AKIONGOZA KIPINDI CHA MAOMBI SIKU YA JUMAPILI 05.02.2017 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 05.02.2017 Mch. Noah Lukumay wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linaloongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuongoza kipindi cha maombezi na uponyaji. Tunamshukuru Mungu kwani watu waliweza kupokea Nguvu kupitia mtumishi wake Mch Noah Lukumay. Ibada hii ilikuwa ni ibada yenye upako na uwepo wa Mungu kwani tuliona Mungu akiwaponya watu wenye mapepo, majini, magonjwa na shida mbalimbali. Hakika Mungu wetu atabaki kuwa Mungu kwani anatenda matendo makuu kupitia watumishi wake wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". 
 
Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi sa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Utasikia watu wakisema "Kwa Mama Gertrude Rwakatare". Baada ya ibada watu watarudishwa katika kituoni.







 













Comments