28.08.2016: MAELFU WAOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale anayofannya kwa wake. Siku ya Jumapili 28.08.5016 katika tamsha la malombezi lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto, watu wengui wengi waliweza kuokoka na kuongozwa sala ya toba na Mch. Kessy mabye pia ni mzee wa kanisa hili.

Watu walifunguliwa na wengine kupokea Nguvu za Mungu palepale na kujikuta wanaanguka chini. Waliweza kutokwa na mapepo na majini yaliyokuwa yakiwasumbua kwa kipindi kirefu.
Mch. Kessy

Sasa lililobaki kwetu ni kufunga na kuomba juu ya hizi kondoo mpya kwaa maana hawa ndugu zetu wanawindwa na adui shetani kwasababu wamemsaliti na kuja kwa Yesu. Tuspowaombea tutakuwa hatutende haki kwa hawa ndugu zetu. Kumbuka na wewe ulipookoka kuna watu walifunga na kuomba ili usimame kwenye wokovu.

Na kwako wewe ambaye hujaokoka tunakualika Jumapili hii kutakuwa na ibada nzuri sana na tutakuombea na kukuongoza sala ya toba ili kuungama dhambi zako na kuanza maisha mapya.


 















Comments