28.08.2016: DADA KUTOKA SUMBAWANGA MWENYE KIDONDA SUGU APATA UNAFUU BAADA YA KUOMBEWA 21.08.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Ikiwa ni Jumapili ya pili ya tarehe 28.08.2016 dada kutoka Sumbawanga akisumbuliwa na kidonda kilichotoka na kandambili za kimasai ambazo alizinunua, na baada ya kuvaa kidole gumba cha mguuni kikachubuka kidogo,. Baada ya siku chache kidonda kikiaanza kutokea katika eneo la juu ya kidole (kama amavyoonekana kwenye picha).

Dada huyu anasema amezunguka kwa waganga wa kienyeji na mahospitalini kwa muda mrefu na hakupata uponyaji/ Anasema ilifika kipindi akamwambia mama yake haangaiki tena na matibabu kutokana na kutokuwa na pesa kwani mume wake alifariki na hakubahatika kupata mtoto. Ndugu zake wamemsaidia lakini sasa wamebaki kumuangalia tu.

Dada huyu anasema, ndugu zake wa Dar es Salaam waliweza kumpigia simu na kumuomba aje Dar es Salaama kwaajili ya maombezi, na alipofika Dar es Salaam alizunguka makaisa mengi bila kupata majibu. Siku moja akiwa nyumbani kwa hao alikofikia, mmoja wa ndugu yake akamuomba aje kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B". Dada huyu anasema alipoingia hapa kanisani kwanza alijisikia ubaridi katika mwili wake, na pia alishangazwa kusikia Mch. Noah Lukumay akiita watu wenye vidonda mguuni kuombewa. Na alipoombewa alijisikia mwepesi na maumivu kupungua kabisa,

Dada huyu hajakata tamaa na anazidi kuja kanisani kwa maombizi. Picha hii ni ya Jumapili yake ya pli kukanyaga katika kanisa hili.

Comments