28.08.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AMRUHUSU MARTHA KOMANYA KUANZA HUDUMA YA KUONGOZA PRAISE & WORSHIP TEAM BAADA YA KUSIMAMISHWA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 28.08.2016 katika tamasha la maombezi aliweza kutangaza rasmi kuruhusiwa kwa mwimbaji wa Praise and Worship Team wa kanisa hilo Martha Komanya kuanza rasmi huduma yake ya kumtumikia Mungu baada ya kufungiwa kwa kipindi kama cha mwaka mmoja baada kutokana na kutengana na mume wake, na hivi ndivyo alivyosema, “Nimeona ya kwamba Martha Komanya tumruhusu aanze huduma ya uimbaji na ninaomba sasa tumuweke mikononi mwa Mungu ili aweze kutumika katika uimbaji tunaachilia uwepo wake wa Bwana juu ya mtumishi wake huyu.” Baada ya hapo waliweza kumuombea na kumruhusu kuanza huduma yake ya uimbaji. Pia aliwaomba waamini wa kanisa hilo kumuombea ili azidi kudumu katika kazi ya Mungu.


Comments