28.08.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ACHUKIZWA KUONA WATU WAMEFUNGWA NA SHETANI KATIKA TAMASHA LA MAOMBEZI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI SIKU YA JUMAPILI

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na hasira kuona watu bado shetani anawatumia na wengine wanajiita wameokoka lakini bado shetani amewakwida kooni, alianza kwa kusema, “Bwana Yesu apewe sifa, Tulisema habari ya Ngamia, Ngamia ni mnyama ambaye anatumikishwa kubeba mizigo. Ngamia hata kama hapendi lakini utakuta kabebeshwa mzigo kwa sababu amefungwa nira, anaendeshwa na watu wengi, hataki kufanya kitu lakini analazimishwa na anajikuta amefanya. Watu hawataki kulewa lakini wanalewa kwa sababu kuna kamba imefungwa shingoni mwao na wanashindwa kuachia wanaenda popote wanapoambiwa. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Watu wamebebeshwa mizigo mizito bila mishahara na hakuna mtu wa kumlalamikia, watu wanatumikishwa na mizigo ya shetani, anatumikishwa na ulevi, ukali yaani mtu mkali kama hajaokoka hadi unajiuliza, ”Huyu mtu ana Roho wa Mungu kweli? Lazima vifungo hivi vifunguliwe watu wakikuona wajue kweli umeokoka. Tunajua Mch. Noah Lukumay ni Mmasai, jamani tumepata Mmasai bora. Kumbuka Wamasai wanavaa lubega na wanatembea na mkuki au fimbo au lungu, lakini ukimuona Mch. Noah Lukumay huwezi kujua kama Mmasai lakini ni Mmasai. Jamani huyu ni Mungu kambabirisha mchungaji wetu. Kama wewe ni Mkulya ukiokoka ukali uache. Lakini watu bado wamefungwa na mikataba ya mila, hat a kama wewe ni Mchaga acha unyimi ( pesa yako ni yako na ya mwenzako ni yako).

Jamani watu wakiokoka wanaachaga hizo mila!!. Wenzako wanaenda kwa waganga, kwa wafundi, lakini wewe fundi wako ni Yesu kristo. Funga mikataba ya dini ulikotoka, kama kuna mikataba ya magonjwa , tunaivunja. Acha tabia ya kupiga mke wako. Jitahidi sana kuwa mtu wa kanisani, na Jumapili hii saa 3 asubuhi tunakualika ibadani. Mungu akubariki sana





Comments