19.07.2016: PRAISE AND WORSHIP TEAM YAONGOZA KIPINDI CHA SIFA KATIKA SEMINA YA WIKI YA KUKUMBUKUKWA SIKU YA JUMANNE MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Praise Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" iliweza kuongoza kipindi cha kusifu na kuabudu katika semina ya " Wiki ya kukumbukwa na Mungu (A week to Remember) inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 10 jioni na kuendelea. Semina hii ambayo itahitimishwa Jumapili 24.07.2016 ilifunikwa na uwepo wa Mungu kutokana na zile nyimbo zilizokuwa zikiimbwa katika kipindi hiki cha sifa. Watu waliuguswa na huduma hii ya uimbaji na kusababisha wengine kujazwa Roho Mtakatifu. Ikiwa leo tarehe 19.07.2016 ni siku ya tatu tangia semina imeanza, watu wanazidi kumiminika katika kanisa hilo kutokana na kile wanachokipata na kukipokea kutoka kwa watumishi wa Mungu.

Mnenaji wa semina hii Mch. Amosi Holilo alionekana kuguswa na uimbaji wa Praise and Worship Tean na kuonekana mwenye furaha. Tunakushauri wewe ambaye hujafika jitahidi ufike kwani utajifunza vitu vizuri sana. Mungu akubariki na leo tukutane ibadani.
 
 


 
 
 
 


 
 
 




















Comments