22.05.2016: MZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO APOKEA UPONYAJI WA TATIZO LA GANZI KATIKA MKONO WAKE SIKU YA JUMAPILI



Siku ya Jumapili 22.05.2016 ambayo ilikuwa ni siku ya UKOMBOZI, Mzee wa kanisa aliweza kufika katika madhabahu ya Mlima wa Moto na kushuhudia jinsi Mungu alivyoweza kumkomboa katika tatizo lililokuwa likimsumbua katika mishipa yake iliyokufa ganzi, alisema “Mhhhh...jamani Mungu anatushangaza, mimi nilipatwa na tatizo la ganzi mkono wangu wa kushoto kwa kipindi sasa, lakini maombezi yalipokuwa yanaendelea hapa ibadani nikaona mishipa inasimama na ganzi imepungua. Mungu ni mwema, ninaimani ipo siku nitatembea bila maumivu tena.
Baada ya hapo Mch. Noah Lukumay aliongoza maombezi akishirikiana na wachungaji na waumini wa kanisa hilo wakiwa wamenyoosha mikono madhabahuni aliko huyu mama na alisema, “Baba tupo chini ya miguu yako, tunaomba umrudishie nguvu katika mifupa na mishipa, Wewe ni Bwana utendae Ishara na Maajabu, ninaachilia neema yako ikatembee juu yake Bwana, kwasababu kazi njema uliyotenda ni kubwa. Hakuna mtu atendae miujiza ila ni wewe. Amen

Comments