29.05.2016: MAMA MTEVU AMSHANGILIA YESU KRISTO MADHABAHUNI BAADA YA KUPOKEA UPONYAJI

Mama Mtevu aliweza kumshukuru Mungu kwa kumrejeshea nguvu baada ya kuteseka kwa muda mrefu. Siku ya Jumapili 29.05.2016 aliweza kucheza mbele ya madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini dar es Salaamna kuwashangaza waumini kwani hawakutegemea kumuona akicheza kutokana na kuumwa kwa kipindi fulani. Jumapili iliyopita alikuja madhabahuni akiwa ameshikiliwa kwaajili ya maombezi, na kanisa zima liliweza kumuombea.


Mama Mtevu amekuwa ni nguzo katika maendeleo ya kanisa jipya la Mlima wa Moto Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa kujitoa na kujinyima kuhakikisha kila Jumapili anatoa mchango wake. Ila Jumapili hii alifanya surprise kubwa sana kwa kuonekana anacheza muziki akimshukuru Mungu kwa furaha na aliweza kumtolea Mungu sadaka kubwa sana na kusababisha watu kuguswa na kumuunga mkono akiwemomzee wa kanisa mama Mshobozi ambaye alitoa nusu ya ile pesa aliyoahidi mama Mtevu.

Tunajifunza mambo mengi sana kupitia mama mtevu kwa jinsi alivyomvumilivu na sio mtu wa kukata tamaa. Kipindi anaumwa amekuwa akijibidiisha sana kumtolea Mungu na kuhudhuria ibada, na watumishi wa Mungu wakiongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wamekuwa wakimuombea madhabahuni ili Mungu amponye.

Hakika Mungu aliweza kusikia maombi ya watumishi wake na maombi ya mama Mtevu, na leo hii anafurahia uponyaji aliopta katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".

unaweza na wewe unapitia matatizo makubwa zaidi ya mama Mtevu, usikate tamaa na ujitume kumtolea Mungu na kuhudhuria ibada za kanisani. Kama huwezi kufika kanisani kutokana na ugonjwa wako, jitahidi kuwaomba watu wakusaidie ufike nyumbani mwa Bwana ili uombewa kama mama Mtevu alivyokuwa akifanya kipindi anaumwa. Na kama imeshindikana kabisa waombe watumishi wa Mungu wakutembelee wakuombee na pia uzidi kumuomba Mungu bila ya kukata tamaa. Kumbuka kila kitu kina mwanzo na mwisho chini ya hili jua. Kwahiyo ungonjwa wako una mwisho wake

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lipo wazi na linampokea kila mtu, kila kabira na ni la kwa dini zote.

Tunakualika Jumapili hii ya HABARI NJEMA kuanzia saa 3 asubuhi na kuendelea..







Comments