24.04.2016: UBATIZO: HAIJALISHI UNAPITIA MAPITO GANI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika huduma yake ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Siku ya Jumapili 24.04.2016 watu waliweza kujitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" baada ya Mch. Otieno kuwaita wale wote wanaohitaji kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao. Tunamshukuru Mungu watu wengi sana walijitokeza na na waliongozwa sala ya toba na Mch. Mama Mgeta na hatimaye kupelekwa baharini kwaajili ya kubatizwa.

Kwa wiki hii watakuwa katika mafundisho ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam.

Wewe ambaye hujaokoka, sauti ya Mungu inakuita njoo uokoke kwani hujui kitu gani kitakutokea baadae kuanzia sasa. Itafika kipindi utatamani kufanya kazi ya Mungu lakini itashindikana kutoka na tatizo ulilonalo. Ni wakati wako mzuri sana wa kutumia karama yako kipindi hiki cha ujana wako, utoto wako, uzee wako kwani Mungu anakuhitaji sana katika kuujenga mwili wa Kristo.

Mungu akusaidie ujumbe huu ukuguse na uokoke kwa Jina la Yesu Kristo.

Ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" inaanza saa 3 asubuhi kila Jumapili na usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini Dar es Salaam au Mwenge mataa utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", ingia humo.

UJUMBE WA MUNGU KUTOKA KWA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

HAIJALISHI UNAPITIA MAPITO GANI
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 24.04.2016 katika somo alilokuwa akifundisha alisisitiza juu ya kutojali mapito tunayopitia na tujitahidi kuwepo kanisani, na hivi ndivyo alivyosisitiza, “Mimi ninakupenda na Yesu anakupenda haijalishi unapita katika shida gani, haijalishi umepita katika misuko suko gani,  MUNGU yuko na wewe imetosha. Kaa na matarajio nakuhakikishia MUNGU atashuka mahali ulipo, unaweza usisikie kama amekugusa lakini unaweza ukasikia kama kaubaridi kamekugusa, au unaweza ukasikia kama moto umekupitia ujue hyo ndio MUNGU anakugusa. Jamani MUNGU yupo, MUNGU anaweza, MUNGU anajibu, tumemuona MUNGU wengine hatukuwa hivi jamani ila ni MUNGU tu anayetutengeneza. Mara nyingi naawaza bila MUNGU tungekuwa wapi? MUNGU atuhurumie, MUNGU akukumbuke, MUNGU akutane na haja ya moyo wako, MUNGU akupe faraja ya tofauti, BWANA Yesu apewe sifa. Maana tuliambiwa msiache kukusanyika kama ilivyo desturi ya watakatifu, sasa ukiona mtu hakusanyiki na hana sababu basi uwe na mashaka naye na ujiulize ni nini kinamfurahisha, kama siyo kuwemo nyumbani kwa BWANA. Kama wewe una udhuru na huwezi kufika katika nyumba ya BWANA, MUNGU si anakuona!!, lakini wengine hata hawana udhuru yuko tu nyumbani kwake siku ya Jumapili au katika kati ya wiki wakati wenzake wako kanisani yeye  anazunguka zunguka tu nyumbani kwake, anaweza akaingia chumbani akatoka, mara akaingia jikoni akatoka, mara anaanika nguo, unakuta mtu anazurura kwenye nyumba yake, sasa hiyo roho ya kuzurura nyumbani kwako wakati wa ibada ishindwe kwa jina la Yesu Kristo. Kila mtu siku za ibada anatakiwa kuwepo kanisani ndipo utaona Mungu akikushindia katika majaribu unayopitia. Kanisani utajifunza vingi kutoka kwa Mungu kwa kupitia watumishi wake aliowaandaa siku hiyo kwaajili yako. Una kifungo, una shida, mambo hayaendi  njoo nyumbani mwa Bwana hata kama unaumwa majibu yako nyumbani mwa BWANA. Siku Bishopo wenu (Dr. Gertrude Rwakatare)  nilikuja hapa kanisani ibadani nikiwa nimebanwa na kihoma na kimenikuda; sasa unajua wachungaji hawasemagi wanaumwa basi nikaja hapa madhabahuni  nikakaa pale na angalia watu sijui kama wananiona. Wakati wa kipindi cha sifa, watu  wakiucheza na mimi nikawa najitahidi kidogo kucheza, lakini nimebanwa nikasema heri kufia madhabahuni kuliko nyumbani. Mchungaji Lukumay akaanza kuhubiri nikasikia jasho linanitoka,  halafu mtoto mmoja mzuri sana akaniletea maji ya kunywa, yana chengachenga za ubaridi, nikasema hivi huyu aliona nini, nikanywa na nikajiona niko sawa. Mungu yupo jamani. Usikose ibada ya Jumapili Mlima wa Moto saa 3 asubuhi.

































































Comments