24.04.2016: MAOMBEZI: KAA KATIKA UWEPO WA MUNGU


Siku ya Jumapili 24.04.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakare katika ibada iliyofanyika Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini dare Dar es Salaam aliweza kusisitiza juu ya watu kukaa katika uwepo wa Mungu na wataona mkono wa Mungu ukiwabariki, na hivi ndivyo alivyosisitiza, “Namuonea wivu ndege mbayuwayu aliyetengeneza kiota chake mbele za BWANA, maana kila wakati wakiimba anasikia uwepo wa BWANA, wakati watu wakiomba uwepo wa BWANA ukishuka na yeye unamshukia. Heri yeye mbayuwayu anayedumu nyumbani mwa BWANA kuliko mimi ninayekaa kwenye Ikulu. Heri wewe na mimi leo tuko nyumbani kwa BWANA, kaa na matarajio, wewe uliyekawia kupata mume, wewe uliyekawia kujenga, unanyanyasika, umekawia kuendesha gari yako, unasema hivi na mimi ni lini neema hii itanishukia, nataka nikuambie kuwa uko mahali sahihi unapokuwa nyumbani mwa BWANA ni lazima MUNGU atakushushia baraka kwako.
Leo ni siku ya muujiza wako, tumekuwa na siku tatu za kufunga na kuomba, kwa ajili ya maombi ya kufunguliwa watu, yalikuwa ni maombi ya siku tatu za urejesho, na mimi nina uhakika MUNGU atakurejeshea kila kitu ambacho wewe umepoteza, unaweza kuwa umepoteza furaha, hauioni tena ile furaha ya zamani, yaani wewe ni mtu ambaye upo upo tu hata chakula unakula basi tu kwa ajili ya njaa lakini ile raha imepotea. Nakuambia mara baada ya ibada hii ile furaha ya Roho Mtakatifu ikurudie tena kwa Jina la Yesu.
Naongea na wewe mwenye huzuni una jambo lako limekuzidi na hujui hata umwambie nani umelia mpaka machozi yamekauka mpaka ukasema ngoja nijiendee tu kwenye ibada nikafarijke, nakwambia uko mahali sahihi na kumbatio la BWANA nimeliona, BWANA atakukumbatia, BWANA atakuambia usiogope, niko pamoja na wewe, Bwana atakuambia jipe moyo, endelea mbele. Bwana asifiwe sana. Uko mahali pa kupokea faraja. Mikutano ni mingi tunahudhuria, mikutano mingi tunaondoka na huzuni, wengine wanaondoka na manung’uniko, wengine wanaondoka na ngeu. Lakini mkutano huu Mtakatifu wa Mlima wa Moto utaondoka na Baraka, ni mkutano Mtakatifu ambapo ni lazima utaondoka na kicheko, MUNGU hawezi kukuacha kama ulivyoingia utoke hivyo hivyo, hutatoka kama ulivyoingia japo hausikii kitu lakini ndani kutakuwa kumetendeka kitu ambacho kitakubeba kwa wiki nzima. Usikose ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi Mlima wa Moto Mikocheni ”B”


BAADA YA BISHOP DR. GETRUDE RWAKATARE KUMALIZA KUHUBIRI YALIFUATA MAOMBEZI NA UPONYAJI













BAADA YA IBADA KUMALIZIKA MCH> NOAH LUKUMAY ALIWEZA KUWAOMBEWA WATU WENYE UHITAJI




















 Dada mwenye jina mahaba akiombewa




 Dada mwenye jini mahaba akiombewa
 mama huyu alikuwa akisumbuliwa na kitu tumboni kwake

Comments