10.01.2016: WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO WAKISALIMIANA

Siku ya JUmapili 10.01.2016 katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" waumini wa kanisa hilo walipata muda wa kuweza kusalimia kabla ya kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wao,Hii inaonyesha ule upendo wa Agabe kama tunavyosoma katika vitabu vitakatifu. Ibada ilifunikwa na wingu la uweopo wa Mungu, na baada ya zoezi la kusalimiana kuisha waumini walipata muda wa kusifu, kuabudu, kusikiliza shuhuda mbalimbali na pia kusikiliza neno la Mungu kutoka kwa wachungaji wa kanisa hilo na pia Neno la Uzima kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Tunakukaribisha sana katika Ibada za Jumapili zinzoanza saa 3 asubuhi. Usafiri wa kufika ni bure, unatakiwa kufika katika kituo cha Mabasi Makumbusho, nje kidogo utaoma basi lenye label ya kanisa hili. Ingiia humo na hakuna atakayekusumbua






Comments