WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B WAKIFANYA MAOMBI SIKU YA JUMAPILI

Hii ilikuwa ni ibada ya kipekee siku hii ya Jumapili ambapo watu waliweza kumuomba Mungu kwa namna ya tofauti sana. Mungu wetu anazidi kuonekana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Assemblies of God kwa Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare.


Siku ya Jumapili watu waliweza kufanya maombi mafupi kwaajili ya kuiombea SHILOH TANZANIA 2015 ambayo itaanza rasmi siku ya Jumapili 06.12.2015 na kumalizika siku ya Jumapili 13.12.2015 na itakuwa ikianza saa 10 jioni na kumalizika usiku.


Katika Shiloh hii kutakuwa na mambo mengi sana, na baadhi yao ni watu kupata muda wa kushuhudia matendo makuu ya Mungu waliyofanyiwa katika Shiloh Tanzania 2014, kutakuwa na uimbaji kutoka kwa waimbaji maarufu sana Tanzania kama Bahati Bukuku, Gideon Mutalemwa, Goodluck Gozbert, Vocal Akapela, Alice, Happy Choir, Joy Bringers na wengine wengi, kutakuwa na wahubiri kutoka nje ya Tanzania na nchini Tanzania kama Askofu Dastan Maboya., kutakuwa na red carpert, mahojiano katika vyombo vya habari, zawadi za saa kwa wafuatiliaji wa Praise Power Radio, Neno la Mungu n.k.

Kanisa la Mlima wa Moto limekuwa kimbilio la wengi kutoka na nguvu za Mungu zilizotawala mahali hapo. Jumapili hii kwa kupitia uimbaji watu waliguswa na uimbaji kutoka katika kwaya kuu ya kanisa hilo na kufanya watu kutokwa na machozi kwani kwa kupitia uimbaji watu waliona nguvu za Mungu zikiwaajilia katika miili yao.

Askofu Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kutoa Neno la Uzima kwa waumini wa kanisa hili baada ya kipindi cha sifa kumalizka na watu waliweza kubarikiwa sana. Kanisa limefanyika kalakana ya faraja kwa wale wanaohitaji kufarijiwa na pia watu wamekuwa wakifanikiwa katika biashara zao na kazi zao kwa kupitia damu ya Yesu Kristo.

Sasa ni zamu yako wewe amabaye hukubahatika kufika katika ibada hii ya Jumapili, kufika sasa katika Ibada ya kipekee sana ya Jumapili kwani ni Ibada ya kwanza kufanyika mwaka huu ikiwa imebeba nguzo ya SHILOH. Uje na ndugu au jamaa zako nao waweze kufaidika baraka za Mungu kupitia Shiloh hii ya mwaka 2015. Uje ukiamini ya kuwa sasa Mungu anakwenda kutatua matatizo yako.

Jinsi ya kufika panda magari ya Mwenge, shuka Mwenge mataa, uliza watu wa babaji wakufikishe kwa Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare.
Tembelea
www.mountainoffiretanzania.blogspot.com
Facebook: Mountainoffire Tanzania





















Comments