01.11.2015:2015: WAJERUMANI WALIVYOSHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KWA ASKOFU DKT. GERTRUDE RWAKATARE

Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God Mikocheni "B" ni kanisa ambalo limekuwa likiwapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali na kushiriki pamoja katika ibada zinazoendelea katika kanisa hilo. Jumapili hii liliweza kupokea Wajerumani ambao waliweza kupata muda wa kuweza kuongea na waumini wa kanisa hilo. Wageni hawa waliweza kumshukuru Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare kwa kuwakaribisha  na  pia walimshukuru sana Mungu kwa kuwapa neema ya kushiriki ibada hii takatifu.

Kiongozi wao Bwana Daniel aliweza uongea mengi sana na kusema hakika amefurahi sana kuwa pamoja na Watanzania ambao ni wema na wacha Mungu. Akiongea kwa utani alisema Yeye ni Mchaga na ngozi yake sasa imeanza kugeuka na kuwa kama ya wachaga, huu ulikuwa ni utani.
Hakika walionekana kufurahi sana jinsi walivyopokelewa vizuri na waumini wa kanisa hilo. Sasa tuone baadhi ya picha zao.










Comments