SIKU YA JUMAPILI 20.09.2015 KANISA LA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES OF GOD LABATIZA WAOKOVU WAPYA



Siku ya Jumapili 20.09.2015 baada ya Ibada Kuu kumalizika katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God-Tanzania, waokovu wapya waliweza kupelekwa katika bahari ya Hindi kubatizwa. Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa waokovu hawa wapya kwani waliweza kuombewa kabla na baada ya kubatisa.

Baadhi yao waliweza kutokwa na mapepo baada ya watumishi wa Mungu kama Mch. Stanley Nnko kuwaombea na kukata minyororo ya mateso.

Pia watumishi wa Mungu waliwaomba waokovu wapya kutorudi nyuma tena na kufanya mabaya kwani katika safari ya wokovu kuna vipingamizi vingi sana, kwahiyo wazidi kudumu katika maisha ya maombi na pia kushirikia ibada na semina zinazoendelea katika kanisa hili la Mlima wa Moto

. Waliombwa sana kusoma Neno la Mungu ili kujua maagizo ya Bwana wetu kwa kupitia kitabu chake kitakatifu (Biblia). Wazidi kuwa watu wa upendo kwa kuwapenda watu wote na kuwasaidia wenye uhitaji.

Kanisa hili limekuwa likiwabatisa watu wengi na kufundishwa Neno la Mungu ili wazidi kudumu katika kumtumikia Mungu kwa uaminifu. Tumeweza kupata shuhuda nyingi kwa watu ambao waliamua kubatizwa na kuishi katika maisha ya kumtukuza Mungu. Watu wengi sana wamebarikiwa katika biashara zao, ndoa zao, familia zao na sehemu mbalimbali baada ya kumpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yao.

Sasa ni wakati wako wewe ambaye hujapatizwa bado na hujampokea huyu Bwana wetu Yesu kuamua sasa kuja kwa Yesu ili afanyike baraka katika maisha yao. Umeteseka vya kutosha, njoo kwa Yesu sasa upumzike na ufurahie maisha yako ya hapa duniani. Mungu wetu anatamani kukuona wewe ukiwa na furaha, lakini anapoona unafanya maovu, Mungu wetu aanachukia. Amua sasa kumfuata huyu Bwana wetu Yesu Kristo.

Karibu katika kanisa la Mlima wa Moto lililopo hapa jijini Dar es Salaam eneo la Mikocheni B kwa Askofu Mh. Dk. Gertrude Rwakatare ufanyiwe maombi na ubatizwe kwa maji mengi ili ufanyike kiumbe kipya na uzaliwe kwa mara ya pili.

Ukitaka kujua mengi kuhusu kanisa hili tembelea
www.mountainoffire.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com

























Comments