Askofu Maboya kutoka Arusha na
Askofu Mrisa Kutoka mwanza wakikata utepe kuhashiria uzinduzi rasmi wa Shilo
Askofu Maboya, Mchungaji msidizi wa Mlima wa Moto Noah Lukumay na mchungaji kiongozi wa Mlima wa Moto Dk. Getrude Rwakatare wakiliombea taifa.
Mwalimu wa nyimbo za Injili
Afrika mashariki bwana John Shabani akiongoza uimbaji wa wimbo maalum wa Shilo
Mheshimiwa Mary Mwanjelwa (Mbunge
CCM viti Mbeya), akihusika kikamilifu katika kuliombea taifa
Watumishi mbalimbali wa serikali
wakiwemo mawaziri wastaafu wkiwakilishwa na wziri Kihula, wakurugenzi, mameneja, wabunge, waalimu, madaktari,
wanasheria, wanajeshi wakiombewa ili kuwawakilisha wafanya kazi wote wa serikali
Vyombo mbalimbali vya habari
navyo vimeshiriki kikamilifu
Mama Getrude Rwakatare
akimkabidhi kipaza sauti Askofu Maboya kwa ajili ya Neno na maombezi
Kwa mara ya kwanza kongamano la kimataifa la Shilo limezinduliwa Tanzania, ni ndani ya kanisala Mlima wa Moto linaloongozwa na Dk. Getrude Rwakatare.
Hili ni kongamano la kumaliza mwaka
na Mungu na kuanza mwaka na Mungu, ni kuanzia tarehe 8-15/12/2013. Katika
uzinduzi huo mambo muhimu yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuliombea taifa,
kuwaombea viongozi wa Taifa la Tanzania, kuwaombea wafanya kazi wa Tanzania
pamoja na watanzania kwa ujumla.
Pia katika kuungana na watu
mbalimbali duniani katika kuomboleza kifo cha MzeeNelson Mandela, maombi maalum
yamefanyika kwa ajili ya familia yake na nchi ya Afrika ya kusini kwa
kuondokewa na Mzee wetu Mandela.
Baadhi ya wanenaji katika
kongamano la shilo ni Dk. Gtrude Rwakatare mwenyeji, Askofu Danstan Maboya,
Askofu Eugene Mrisa, Fransis Junior, Mch. Noah Lukumay na wengine wengi. Vyombo
mbalimbali vya habari pia vimehusika kikamilifu katika uzinduzi huo
ulioambatana na maombezi ya taifa
Comments
Post a Comment