NENO LA HEKIMA KUTOKA KWA MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE



Wapo wanaodai "FEDHA/PESA" ndio kila kitu katika Maisha yetu hapa duniani, lakini SIO KWELI. FEDHA/PESA SIO KILA KITU, kwa sababu:-
- Fedha inaweza kununua KITANDA lakini sio USINGIZI.
- Fedha inaweza kununua SAA ya mkono au ya ukutani lakini sio WAKATI, kwa sababu Wakati unapita na hautarudi tena.
- Fedha inaweza kununua CHEO lakini sio HEKIMA.
- Fedha inaweza kununua DAWA lakini sio AFYA, maandiko yanasema, nitakurudishia AFYA asema Bwana wa Majeshi.
- Fedha inaweza ununua DAMU lakini sio UHAI.

Tumtegemee Mungu basi kwa kila jambo tunalolihitaji au linalopita katika Maisha yetu ya kila siku. Kumbuka sisi wanadamu tunafananishwa na mnyama au mdudu tu mbele za Mungu kwa hiyo tusijivune kwa lo lote sisi bado ni wahitaji tu mbele zake.

Comments