HIVI NDIVYO KANISA LA MLIMA WA MOTO WAKISHIRIKIANA NA PRAISE POWER WALIVYOTEMBELEA KAMBI YA WAZEE NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI



Baadhi ya mali ambazo zimekabidhiwa kijiji cha wazee, Msimbazi jijini Dar es Salaam.
 


kitendo cha Kanisa la mlima wa moto linaloongozwa na Mama Rwakatare, likishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Redio cha Praise Power Radio kutembelea kambi ya wazee eneo la Msimbazi, jijini Dar es Salaam, na kuwapatia misaada mbalimbali kwa kadri ya uwezo wao, kimepongezwa sana.

Tukio hili ambalo hakika likanikumbusha kuwa kila mtu atazeeka (Kwa Neema), basi likanipa faraja nikijitazama miaka 97 ijayo, na kuona kundi la watu wakitia kambi ghafla kwenye makazi yangu kunipa maneno ya faraja na zawadi mbalimbali, inapendeza.

Tukio hilo limeenda sambamba na mpango wa kanisa hilo wa kutenga mwezi wa novemba kuwa mwezi wa shukrani kwa Mungu. Akiongea kwa furaha, mmoja wa Viongozi wa  Praise Power, Bwana George Mpella,  alisema kuwa msukumo wa kufanya jambo hilo unatokana na Kanisa la mlima wa moto na kituo chao cha Redio, yaani Faraja ya Watu , kwa hiyo licha ya kuwashauri watu kiimani zaidi, pia mwisho wa siku ni muhimu kufanya kitu kama hiki kimwili.

Kuna kinamama wana matatizo ya fistula, wakatengwa na jamii na kuna watoto wana matatizo ya kuwa na vichwa vikubwa - hawa wote wamekuwa wakipata misaada kwa namna mbalimbali, lakini ukiangalia wazee - hili ni kundi la watu waliosahaulika, ndio maana Praise Power Radio - Faraja ya Watu na kanisa la Mlima wa Moto tukafanya jambo hilo, baada ya kufanya utafiti kujua hasa wazee hao wana uhitaji wa aina gani.

Baada ya kufanya hapa, wiki hii wanaendelea - na hapa ni kwa ajili ya wahanga wa kiafya, yaani wale waliojifungua kwa matatizo kwenye hospitali ya CCRBT. Japo hawana pesa nyingi

Mwisho wa yote Bwana Mpella anaiasa jamii ijifunze kukumbuka wasiojiweza, "sisi sote ni vijana, ila mwisho wa yote nasi tutafikia umri huo - hivyo ni vema kujifunza ni mambo gani unaweza kukutana nayo."

Comments