BABA, MAMA NA MKE WA MFANYA BIASHARA WANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KIJANA HUYO KUKIMBILIA KANISA LA MLIMA WA MOTO





 Kibuyu kidogo chenye nembo ya twiga

 Akionyesha moja ya dawa hizo

Maombezi
                               Ni ushuhuda uliosisimua mioyo ya maelfu ya watu waliohudhuria katika ibada jumapili hii. Kijana huyo mfanya biashara wa bidhaa ya duka katika soko la Tandale Uzuri, baada ya kuona biashara yake inalegalega, alipata ushauri wa kuwaona wataalam, ndipo alipomtafuta mganga wa kienyeji na kukabidhiwa dawa mbalimbali.
                          Hakika haijawahi kutokea, katika madhabau ya Mlima wa moto chini ya usimamizi wa Mchungaji Kiongozi Dk. Getrude Rwakatare na watumishi wengine, lilifunguliwa begi kubwa lililokuwa na dawa za aina mbalimbali zikiwepo zile za kuwafanya wateja wasione fremu za watu wengine isipokuwa duka lake. Dawanyingine ni kibuyu chenye picha ya twiga kikiashiria kwamba yeye atakuwa juu kuliko wafanya biashara wenzake na nyingine ya yenye noti zinazoashiria kuvuta pesa kutoka  kwa wafanya biashara wenzake na wateja.
                            Kilichomfanya kijana huyo kukimbilia kanisani usiku wa manane na kuruhusiwa kulala kanisani, ni pale alipopigiwa simu baada ya kuondoka kwamba, awe tayari kutoa damu; na damu hiyo si damu ya mbuzi wala ng’ombe bali damu ya binadamu ambao ni Baba, Mama, ndugu wa karibu na hatimaye mke wake.

                            Kijana huyo aliyekuwa amezilipia dawa hizo malaki ya pesa, alichanganikiwa ghafla na hali yake kubadilika, ndipo alipokimbilia kanisani; na baada ya kuona mlango wa kanisa mida ya saa saba usiku, ndipo hali yake iliporejea kuwa nzuri. Kijana huyo amefanyiwa maombi na sasa Anamshukuru Mungu wa Mlima wa Moto kwa Kumfungua.

Comments