MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE ANAKUKARIBISHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI HII KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD

Mwandishi: Rulea Sanga

Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto anakukaribisha katika ibada itakayofanyika katika kanisa hilo. Kama wewe una tatizo lolote njoo katika nyumba ya Bwana, na Mungu ataenda kukutetea. Wachungaji wamejiaanda kukuombea na kuhakikisha unapata baraka kutoka kwa Mungu. Unachotakiwa ni kuwa na imani ya kuwa Mungu anaweza na kutotenda dhambi. Unaweza kuamini kuwa Mungu atatatua tatizo lako lakiini una dhambi, hapo Mungu hausiki..tubu dhambi zako na usitende tena ndipo utaona baraka zako.
Kutakuwa na Mchungaji kutoka Kenya Francis Junior ambaye amekuwa baraka katika semina inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B. Watu wanabarikiwa na wanafarijika na mahubiri yanayotolewa na mtumishi wa Mungu.
Pia kutakuwa na waimbaji kutoka katika kanisa hilo,Happy Kwaya, Joys Bringers na mwimbaji wa kujitegemea JANE MISO aliyeimba wimbo wa Omoyo.
Njoo na ndugu na jama zako na Mungu atakubariki.
AMEN

Comments