MCHUNGAJI FRANCIS JUNIOR KUTOKA KENYA SIKU YA JUMANNE ALIHUBIRI KATIKA SEMINA INAYOENDELEA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD


Mwandishi: Rulea Sanga
KUDUMU KATIKA BWANA

Tusome Mathayo 15:32-Safari ya kwenda kwa Bwana si rahisi kama unavyofikiri. Mwisho wa jambo ni bora kulioko mwanzo wa jambo. Bwana hawapi watu tunzo ila tu huwapa pale wanapombariki.

Tusome Wafilipi 1:6- Bwana alivyoanza na wewe atamaliza na wewe hata kama kuna wengine walishindwa. Wanaomaliza mbio hizi ni wale wanaodumu katika Bwana. Atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakaye kula tunda la uvumilivu. Yesu alikaa na kusanyiko na ilipofika siku ya tatu jioni, Yesu aliwatazama wanafunzi akasema, “Watu hawa wamekaa na mimi kwa masaa matatu wakinisikiliza.”  Yesu aliwaonea huruma na kuguswa nao.

Mungu anabariki watu alionao,  na wanaodumu katika maombi. Mungu hutumia mtu na kuna wengine watu wanatumia Mungu. Ukitaka mafanikio dumu katika maombi. Omba kila wakati. [Yohana 8:31] Tunapaswa kukaa katika Neno la Mungu matokeo yake ni kuwa wanafunzi wa Mungu kweli kweli. Usisome Neno kama dozi za dawa, bali soma kila wakati na utainuliwa kwelikweli. Watu wanapagawa na mapepo kwasababu hawana Neno la Mungu ambalo linakupa uwepo wa Mungu. Yohana 1:1- Ukijaa Neno umejaa Mungu, mapepo yataondoka yenyewe, na shetani hatakuwepo. Nuru na giza haviwezi kukaa kwa pamoja. Muombe
Tusome Timotheo 1:4:16- Unapaswa kudumu katika mambo ya Mungu na utakuwa nyota inayong’ara. Kwahiyo endelea kudumu katika nyumba ya Mungu kila siku. Mambo sugu katika maisha yako kwa kudumu kwa Neno na kufunga, siku mmoja hayo yote yataondoka.
Mungu anawapenda wote lakini anawapendelea wale wanaodumu nay eye. Yesu alikuwa na wanafunzi 12 lakini aliwachagua watu 3 kwenda mlimani kuomba na alipofika mlimani alimuomba Yohana alale katika kifua chake na kusikia midundo ya moyo wake.

Watu wanaodumu katika kanisa wataambukizwa na kile ambacho kipo katika madhabahu ya kanisa. Unapaswa kudumu katika kazi ambayo Mungu amekupa. Fanya kazi ya Bwana na kutoangalia watu, kama wewe ni mfagizi wa kanisa endelea kufagia kanisa na bila kuangalia watu bali muangalie Bwana.

Wakati unafanya kazi ya Bwana hata kama unachekwa au unapongezwa wewe dumu katika hiyo kazi aliyokupa Bwana. Kama wewe mwimbaji, mfagizi, mtangazaji, msambazaji wa habari kwa njia ya mitandao n.k. endelea na kazi yako. Hakuna mwanadamu anaweza kukulipa kazi unayofanya katika nyumba ya Bwana, ila ni Mungu tu atayekulipa. Hata kama huna mtu anayekushabikia katika kazi ya Bwana wewe endelea na Mungu atakushabikia wewe. Usikubali kuondolewa katika kazi yako ambayo Mungu amekupa. Wewe kama ni mtoaji endelea kutoa mpaka watu wakushangae.
Wenye midomo wataongea lakini wewe fanya kazi ya Bwana na endelea kwa nguvu zako zote.

Bwana anasema anawaonea huruma makutano kwasababu walidumu naYeye mpaka siku ya tatu, kwani walikaa bila ya kula. Mungu hafurahi tu mambo yako uya kiroho bali hata mambo ya kimwili. Yesu aliwaambia mmemaliza mambo ya kiroho na sasa mtapata mkate. Yeyote anayevumilia na karama za kiroho, ataondoka na mkate wa kimwili. Ukimtafuta Mungu utaona utukufu katika sura yako. Endelea kuvumilia kwenda katika nyumba ya Bwana na baada ya hapo utapata mafanikio ya kimwili. “Natamani ukafanikiwe kimwili kama roho yako ifanikiwavyo” Mungu sio ATM kwamba unabonyeza tu na kupata pesa, Mungu ni wa gharama .

Tusome  13:2-Abrahimu alikuwa ni tajiri sana na hakuwa maskini, kwahiyo na wewe hupaswi kuwa maskini. Utajiri unaotokana na wewe kudumu katika Mungu, utanawiri na kustawi.

Miaka itafika ambapo Mungu atainua watu ambao watajenga majumba kwaajili ya wajane na kununua ndege kwaajili kwa kazi ya Mungu. Abrahimu hakuwa tajiri kwaajili ya akili yake ila kwasababu alimpenda Mungu.
Tusome Mwanzo 26:13 – Baada ya Abrahamu kufa, mwanae Isaka alipanda mbegu na akafanikiwa sana. Kama Bwana amekubariki kwa mavazi au gari zuri tumia popote bila ya kuogopa watu, kwani kabla hujabarikiwa na Mungu ulikuwa choka mbaya na leo umeinuliwa, onyesha kuwa Mungu anaweza kubariki watu wanaomtafuata.

Tusome Mwanzo 30:43 Kiroho chako kinahamasishwa na mafaniko yako. Ukidumu katika Neno utafanikiwa katika maisha yako. Bwana akikubarikiwa tembea kifua mbele maana damu ya Yesu imekutoa mbali. Unatakiwa kukaa kama  mtu uliyobarikiwa. Ukiingia katika kanisa kamata roho ya kimataifa ya kufanikiwa. Usiwaonyeshe watu kuwa Mungu wako ni mdogo ila onyesha kuwa Mungu wako ni mkubwa kwa kuonyesha matendo makubwa aliyokubariki.

Yesu aliwaambia wanafunzi kuwa ninyi ndio mtawapa mikate. Mungu anaweza kugusa wanadamu kuwabariki wengine. Mungu huwatumia watu kuwabariki wengine. Silasi aliguswa na Mungu na kuambiwa ajenge kanisa
Tusome Zaburi 45:42- Mungu anaweza kuwatumia matafa (watu ambao hawajaokoka) kuwabariki wengine, wataoa mapesa yao na kukupa wewe mtumishi wa Mungu. Watu wa mataifa watajipendekeza kwako kutoka wewe kudumu katika Bwana.

Maisha ya Dar es Salaam yanaweza kupanda, lakini kwako hayatakusumbua kwasababu umedumu katika Mungu. Mfano Yusufu alipelekewa njiwa na sadaka kutokana na mtoto Yesu. Yusufu aliambiwa aende Misri na Yehova akagusa watu matajiri wauze dhahabu na manemane na kumpelekea Yusufu. Hawakuishiwa chakula. Yusufu aliwashangaza watu wa Misri kutokana na kutafsiri ndoto, baada ya kutafsiri waliona hekima yake na ufunuo alionao, wakaamua kumtafutia sehemu nzuri ya kuishi.

Tusome Mwanzo 41:42- Kuna watu watahama sehemu zao na kukuachia wewe mtu wa Mungu. Farao alipoweka pete katika kidole cha Yusufu kilimtosha. Kuna watu wameshilkilia vitu vyako, na siku ya leo unaenda kuvichukua na wao watakuachilia.

Kazi ya Mungu inafaida na ni nzuri sana, kinachotakiwa ni kudumu katika Bwana. Kwasababu ya kumtumikia Bwana Mungu akulipe.

MUNGU AKUBARIKI

Comments