IBADA YA JUMAPILI KUTOKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD KWA MCHUNGAJI DK. GETRUDE PANGALILE RWAKATARE


Mwandishi. Rulea Sanga

MATANGAZO

MAOMBI YA SIKU TATU KAVU
Mchungaji Rwakatare kabla ya kuanza ibada rasmi aliwaomba waumini wake kufunga siku tatu kavu kuanzia Jumatano ya wiki hii mpaka Ijumaa. Aliwasisitiza sana kutopuuzia swala hili ni la muhimu sana mbele za Mungu. Lengo la mfungo huu ni kuangamiza adui shetani kwa maombi na kuomba baraka kutoka kwa Mungu zitawale katika maisha yetu.

Mchungaji Getrude Rwakatare

SEMINA KUANZIA JUMATATU MPAKA JUMAPILI

Mchungaji Dk. Getrude Rwakatare  aliwatangazia kuwa kutakuwa na semina kuanzia Jumatatu hii mpaka Ijumaa itakayoendeshwa na Mchungaji Francis Junior kutoka Kenya pamoja na Mchungaji Kiongozi Dk. Getrude Rwakatare. Aliwaomba watu wasikose kuja nyumbani mwa Bwana siku za semina.

Mchungaji Francis Junior kutoka Kenya

SHERIA YA KANISA: KUSALI KILA SIKU KUANZIA SAA KUMI NA MBILI KASOROBO
Mbali na ombi hilo, pia aliwatangazia waumnini wote wa Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God kuwa kuanzia sasa kunasheria mpya ya kanisa imetungwa ambayo inamtaka kila muumini wa kanisa hilo kufanya maombi au kusali  kila asubuhi saa kumi na mbili kasorobo, kuliombea kanisa na kujikabidhi kwa Mungu akulinde na mabaya nyumbani kwako au kazini kwako.

SHUHUDA YA MCHAWI
Baada ya hapo kilichofuata ni shuhuda. Waumini wengi waliotoa shuhuda zao na sadaka za shukrani. Lakini katika shuhuda zote, iliyonigusa blogger wenu ni hii ya mama mchawi aliyemua kumkabidhi maisha yake kwa Yesu Kristo. Mama huyu anaitwa Tabia Abdalah ambaye alikuwa mchawi na ameloga wengi sana huko Bukoba na siku ya jumapili yeye na mume wake Zacharia waliamu kumuachia Yesu maisha yao kuwa mwokozi na mkombozi wa maisha yao. Zacharia alisema, “ Alitokea kumpenda sana huyo mke wake kabla hajamuoa, na alipotaka kumuoa, dada hyuo alisema, “Sitaki kufunga ndoa ya Kikristo bali ya Kiislamu”. Mwanaume huyo alikubali kutokana na kumpenda sana na akafunga naye ndoa. Ila siku zilipokuwazinaenda aligundua kuwa mke wake ni mchawi, na baadae wote wakaamua kuja katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B kwa mama Rwakatare kutubu dhambi zao na kuokoka.
Mchawi Tabia Abdalah (wa pili kutoka kushoto) aokoka na kuacha uchawi

Mchungaji Lukumai akionyesha baadhi ya vifaa vya huyo mchawi alivyokuwa anatumia. Karatasi lililoinuliwa ni moja ya silaha ya wachawi

KIPINDI CHA SIFA
Matangazo yalipoisha kipindi cha sifa kilianza na baadae akamwita Malkia wa nyimbo za Injili bahati Bukuku kutumbuiza na kuwafariji waumini kwa njia ya uimbaji. Ilikuwa baraka sana pale mwimbaji huyo alipoimba wimbo wake mpya wa “Dunia Haina Huruma” watu walitoa machozi na wengine walibarikiwa sana.
Bahati Bukuku akimwimbia Mungu

Mchungaji Getrude Rwakatare akicheza wimbo wa "Dunia haina huruma" wa Bahati Bukuku
Mtangazaji wa Praise Power, Erick Brighton akiteta jambo na mmoja wa waumini
Waumini wa Mlima wa Moto wakiufurahia wimbo wa Bahati Bukuku

Mama huyu hapa mbele ni mmoja wa wapokezi wa wageni ofisini kwa Mchungaji Getrude Rwakatare

Mchungaji Msaidizi Lukumai (mwenye suti nyeus) akiongea na Erick Brighton wa Praise Power Radio

NENO KUU LA JUMAPILI
Mchungaji Rwakatare, alimkaribisha Mchungaji Francis Junior kutoka Kenya kuhubiri Neno la Mungu. Katika Ibada hii Mch. Francis ndiye alibeba Neno la Mungu la Jumapili. Neno lenyewe linasema,

KUTENGENEZWA AU KUFANYWA NA MUNGU.

Tusome Isaya 43:19 na Zaburi 118:13, Kuna kitu ambacho Mungu anafanya maishani mwako, hata kama unaona hicho kitu hakijafanyika ila kwa imani kinaenda kufanyika kwako. Kama ni biashara yako iatakuwa ni ya kimataifa. Kile ambacho wanadamu wamesema hakitafanyika ila kwa Mungu kinafanyika. Kwa wale waliompokea Mungu aliwapa uwezo wa kufanya miujiza mikubwa. Tusome Ayubu 14:14. Unatakiwa kuwa mtu wa subira wa kungojea mpaka uone mabadiliko yanatokea na kufanyika. Kanisa la leo limekosa moyo wa subira, kila jambo wataka kufanyika haraka. Kama unataka vitu vya utukufu na vya ajabu unatakiwa kuwa na subirs. Kila unapofanya jambo usimtegemee mwanadamu kwa hana mbingu ya kukupeleka, ila mtegemee Mungu tu ndiye jibu la maisha yako na anaweza kukutengeneza ukawa mtu wa maana katika jamii na mbele Zake.
Dk. Mganga kulia akisikiliza Neno la Mungu kutoka kwa mchungaji Francis Junior kutoka Kenya

Kumbuka ya kuwa, pale mwanadamu anapokuacha, ndipo Mungu anaanzia kukuchukua na kukusaidia. Hata kama watu wanakuvunja nguvu, endelea na safari usirudi nyuma.

Kuna wadada wengune ni wazuri sana na wanauweza wa kifedha lakini hawaolewi, kwasababu hawajatengenezwa na Bwana. Kitu cha thamani katika maisha yako ni kujua Neno la Mungu kwa njia ya Biblia na sio kitu kingine. Moyo wako unatengenezwa kwa kusoma Neno la Mungu na sio kufika kanisani kila siku.

Leo kuna watu wanapenda ibada kuliko wenye ibada na kuna wengine wanapenda miujiza kuliko wenye miujiza na hawapendi kusoma Neno la Mungu ambalo ndilo hitimisho la kila kitu. Tunatakiwa kuwa na roho ya kumtamani Mungu. Ukitaka kuwa mbali na Mungu kaa mbali na Neno la Mungu. Ni hasara kubwa kumjua sana mchungaji wako kuliko kumjua Mungu. Watu wengi wamekuwa karibu sana wachungaji wao ili wasifiwe na hawafanyi yaliyo ya Mungu.

Mungu anataka kizazi kinachomtafuta Mungu na kukataa maisha ya uasherati na maovu yote.  Kuna baadhi ya waimbaji wanakuja kuimba madhabahuni lakini wametoka kufanya uasherati, hili ni chukizo mbele za Mungu.

Mungu aliumba mwanadamu kwa udogo na hakuumba kwa dhahabu na fedha, lengo lake alitaka kuonyesha uwezo wake kuwa Yeye anayaweza yote, kumbuka udongo hauna thamani sana ukifananisha na dahahabu na fedha, lakini Mungu aliutumia kukuumba wewe na leo unaonekana mwenye thamani. Mwanadamu amemusahau Mungu, kanisani anafanya maombi au kusali huku mikono yake ameweka mfukoni, watu hataki kufika kanisani kuomba.

Wanadamu wa sasa wanashangza sana, leo hii mtu anakuwa karibu sana na Mungu pale anapokuwa hana kitu “Choka mbaya” lakini akipata anamsahau Mungu wake. Watu siku ya Jumapili wanajaa sana kanisani lakini siku za katikati ya wiki hawfiki kabisa, ukiwauliza wako busy na maisha.

Mungu wangua akikubariki siku ya leo jaribu kuwa mnyenyekevu na jiachilie Kwake.

Kumbuka ndugu yangu, ipo siku inakuja ambapo mali zako hazitakusaidia lolote, utatamani kusoma Neno la Mungu lakini utashindwa, utatamani kutoa sauti lakini haitawezekana, utatamani kula chakula lakini hutaweza, utatamani kuomba lakini hutapata muda huo, utatamani kumuona mchungaji lakini atakuwa mbali na wewe, utatamani kufika katika mikutano lakini utashindwa, utatamani kuongea na ndugu yako lakini haitawezekana…Muda huu ni muda wakufanya kazi ya Mungu mpendwa wangu

Soma Isaya 41:14

MUNGU AKUBARIKI

Comments