CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mwandishi: Rulea Sanga


KITABU CHA MARKO

SEHEMU YA TATU
Jibu maswali yote kabla hujaangalia majibu ambayo umepewa baada ya maswali

MASWALI

1.      (i) Yesu aliwahurumia makutano kwa kutokula chakula kwa muda wa siku tatu tangia amekuwa nao. Kwanini Yesu aliogopa kuwaaga bila ya kuwapa chakula?

(ii) Wanafunzi wa Yesu waliopomjibu Yesu kwa kuuliza swali, Je! Atawaweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate nyikani?, Je, Yesu aliwajibuje?

(iii) Yesu alifanya nini baada ya Yesu kujibiwa kuwa wanayo mikate saba na visamaki vichache?

(iii) Je, wanafunzi walishiba hiyo mikate saba na visamaki vichache?

(iv) Watu wangapi walikula hiyo mikate saba na visamaki vichache?

2.      Mafarisayo walipokuwa  wakihojiana na kutafuta ishara itokayo mbinguni, Yesu alisema nini juu ya hilo jaribu? 

3.      (i) Kwanini Yesu alisema maneno haya “ Je, mioyo yenu ni mizito? Mna macho hamuoni, mna masikio hamsikii? Wala hamkumbuki?”

4.      (i) Yesu alifanya ishara gani alipomponya yule kipofu Bethasaida?

(ii) Yule Kipofu alipoulizwa Je, Waona? Alimjibu nini Yesu?

(iii) Yesu alipojibiwa lile swala la Je, Waona?, nini alikifanya tena kwa huyo kipofu?

5.      Yesu alienda na nani mlimani ambako aligeuka sura yake, mavazi yake yakawa meupe mno yakameta-meta?

MAJIBU
1.      (i) Kwasbabu aliona watazimia njiani ni baadhi yao walitoka mbali. (Marko 8:1)

(ii)  Yesu aliwauliza, Mnayo mikate mingapi? (Marko 8:5)

(iii)  Yesu aliwaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wakewawaandikie, wakaawandikia mkutano. Akavibariki visamaki vile vichache, akasema wawaandikie nahivyo pia. (Marko 8:6-7)

(iii) Ndiyo, walikula wakashiba wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. (Marko 8: 8)

(iv) Watu waliokula yapata elfu nne. (Mako8:9)

2.      Aliwambia, “Mbona kizazi hiki chatafuta isahara? Amini nawambia, Hakitapewa ishara kizazi hiki” (Marko 8:12)

3.      Kwasababu wanafunzi wake walikuwa na wasiwasi kutokana na kutokuwa na mikate ya kutosha baada ya kusahau kuibeba na walikuwa na mkate mmoja tu katika chombo chao. (Marko 14)

4.      (i) Yesu akamshika mkono na akamtemea mate ya macho, akamuwekea mikono yake . (Marko 8: 23)

(ii) Alimjibu, Naona watu kama miti inakwenda. (Marko 8:24)

(iii) Yesu aliweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana, akawa mzima, akaona vyote waziwazi. Marko 8:25)

5.      Yesu alienda na Petro, Yakobo na Yohana.(Marko 9:2)

Comments