MCHUNGAJI RWAKATARE AKICHEZA NA WANAFUNZI WA ST. MARYS
MCHUNGAJI Getrude Rwakatare ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa shule za Kimataifa za Mtakatifu Maria (St Mary), mwishoni mwa wiki iliyopita alilisakata Sebene la Yesu katika mahafali ya shule ya St Mary iliyopo maeneo ya Kihonda mkoani Morogoro.
Mchungaji huyo ambaye pia ni Mbunge ya Viti Maalum CCM (Kilombero) Mkoani Morogoro, alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la awali (chekechea) yaliyofanyika Ijumaa shuleni hapo.

Baada ya kuwatunuku vyeti wanafunzi hao, mchungaji huyo alijimwaga kwa kucheza muziki wa Injili na wanafunzi hao.
 
Katika hotuba yake, aliwataka wazazi kutojikita zaidi kwenye mambo ya kuchangia kadi za harusi badala yake wajikite zaidi kwenye masuala ya kuwasomesha watoto wao.
 
Picha zifuatazo zinasimulia tukio hilo:


Mchungaji Rwakatare akicheza na wanafunzi
Mchungaji Getrude Rwakatare (wa kwanza kushoto) akicheza Sebene la Yesu katika mahafali ya shule ya St Mary iliyopo maeneo ya Kihonda mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.



Comments