MCHUNGAJI RWAKATARE ANAKUKARIBISHA KATIKA IBADA YA JUMAPILI KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHEN B ASSEMBLIES OF GOD
Mwandishi: Rulea Sanga
Mchungaji anakuomba wewe Mtanzania kufika katiKA IBADA YA Jumapili
katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B. Ibada itaanza saa 3:00am.
Anakualika kufika pamoja na jamaa zako ili kumsifu na kumtukuza Mungu.
Mungu anapenda kuona wewe unamtumikia kwa upendo na bila ya kusukumwa na
mtu yeyeyote.
Ni mengi utayapata katika nyumba ya Bwana, na hayo utayapata kutoka na
imani yako na utayari wa moyo wako. Njoo mpendwa tumtukuze Mungu wetu.
Huu ni wakati wako wa kufanya kazi ya Mungu, itafika siku utashindwa
hata kunyanyua kijiko au kutoa sauti, utatamani kusoma Neno la Mungu
lakini utashindwa.
Mimi kama mchungaji nategemea utafika na hutaniaabisha mtumishi wako.
Jinsi ya kufika, panda magari ya Mwenge, na ukifika Mwenga uliza njia ya
kwenda katika kiwanda cha Coca Cola, hapo utaona Bajaj nyingi na pia
utaona mabasi ya St. Marry's secondary School, yatakuleta kanisani bure.
Jumapili hili kutakuwa na uzinduzi wa albam ya Happy Choir ambao utafanyika hapo kanisani kuanzia saa 9:00. Hakuna kiingilio
Waimbaji katika ibada ni Happy Choir na Joys Bringers
Comments
Post a Comment