MCHUNGAJI RWAKATARE AMRITHI SALOME MBATIA


Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana chini ya Mwenyekiti wake,Rais Jakaya Kikwete,imemthibitisha Mchungaji Dr.Getrude Rwakatare kuwa mbunge wa viti maalumu,kurithi nafasi ilioachwa wazi na marehemu Salome Mbatia aliyefariki Octoba mwaka huu kwa ajali ya gari.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar jana mara baada ya kikao cha kamati kuu,katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi,Bw.John Chiligati,alisema kufuatia uamuzi huo, mchungaji Rwakatare sasa ni Mbunge mteule akisubiri kuapishwa wakati wa mkutano ujao wa Bunge utakaofanyika januari mwakani

Comments