MCHUNGAJI KYANDO WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ALIVYOFUNDISHA JUU YA NIDHAMU KATIKA MAOMBI TAREHE 5-10-2008 KATIKA KIPINDI CHA SUNDAY SCHOOL

Mwandishi: Rulea Sanga (RUMA AFRICA)

Bwana Asifiwe watu wa Mungu!! .Tusome katika (Methali 1:1-7)

Tunajifunza ili tupate hekima na kutembea kwa adabu. Mungu anasema watu wangu wanakosa kwa kukosa maarifa. (Malaki 1:6) Kumcha maana yake ni hofu, tunatakiwa kumheshimu Mungu tunaposogea katika maombi. Maisha ya waliokoka ni maisha ya maombi. Ukiona kiwango cha maombi kimebadilika katika maisha yako ujue kuna kitu Mungu anataka kufanya, Mungu anataka kukuhamisha mahali pengine kiroho na kimwili. Nadi ya hayo maombi lazima kuwe na adabu na heshima (Isaya 66:2).

Mtu mwenye unyonge na mnyenyekevu, kujalia, upole, Mungu ansema huyu huyu ndiye nitakaye mkubali

Mambo ya kukumbuka tukiwa katika kiti cha enzi (Waebrania 10:19-22)
  1. Tunapokuwa katika maombi tunakuwa tumekaa patakatifu pa watakatifu. Patakatifu ni mahali pa kiti cha enzi cha Mungu
  2. Tunapokuwa tunaomba tunakuwa tumehama katika kiti cha kawaida na kuwa katika kiti cha enzi (patakatifu pa watakatifu).
  3. Mungu hachagui namna ya kuomba, unaweza kuomba kwa sauti au kimia kimia ili kutowakwaza wenzako. Angali mfano wa Esta 5:1-2 jinsi wanadamu wanavyonyenyekea wanadamu ambao ni wafalme

Mambo ya kuangalia unavyokuwa katika maombi:-
  1. Kutenga muda maalum wa kuongea na Mungu, kwa mfano usiku. Usiku malaika huwa wanapita na kuangalia wanaoomba na kuchukua record zao na kuzipeleka mbinguni. (Zaburi 134:1-3 na Matendo 3:1). Mitume wa Yesu walikuwa na utaratibu wa kuomba saa tisa usiku.(Daniel 6:10, Zaburi 34:7). Malaika hutua kwa yule aliyekuwa katika maombi
  2. Kutenga muda wa kumaliza maombi. Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu (Wakoritho 1:14:40). Hata kama umechoka ni lazima kuomba. Mungu anataka tujifunze kuomba kwa muda mrefu.

MUNGU AKUBRIKI KWA HAYA MACHACHE, NATUMAINI YATAFANYA BARAKA KWAKO

Baada ya mafundisho ya Maombi, baada ya hapo likafuata Neno Kuu kutoka kwa Mchungaji Getrude Rwakatare wa Mlima wa Moto Mikocheni B Asemblie of God.

WEKA AGANO NA MUNGU
Bwana Yesu asifiwe, Tusome katika kitabu cha Yohana 8:3-11)
  • Mungu anasema hata mimi sikuhukumu bali usitende dhambi tena. Katika safari  yoyote ya kwenda mbinguni kuna mabonde na milima.

  • Lazima kusimama kuitetea dhambi isitutawale. Chimbuko la dhambi kwa mwanadamu ni mwili. Watu wanahangaika kutafuta maisha kwa kutumia njia zisizofaa. Tusome Wafilipi 4:3, tunayaweza yote kwa yeye anitiae nguvu (ayubu 31:1)
  • Tunapopanga kumshika Mungu ni vizuri kuweka agano na Mungu.
  • Tunapaswa kuacha wivu kwa maana ni dhambi. Hutatakiwi kuwa na wokovu wa uchotara. Kunauwezekano wa kutotenda dhambi (Petro 1:1:15-16).
  • Tunatakiwa watakatifu kama Mugu
  • Tukimkiri Bwana kuna mabadiliko yatatokea katika marafiki kazini, ofisini au mahali popote uendapo. Tunatakiwa kuangalia sana marafiki wa zamani ambao hawajaokoka kwa maana watasababishia dhambi (matendo 4:29, Wagalatia 2:20, 6:14, na 5:16)
  • Tamaa za mwili ni hizi:- Ulawiti, wivu, chuki, usinzi na nyigine kama hizo (Zaburi 119:11
  • Tunatakiwa kusoma Neno la Mungu kwa wingi (Warumi 12:1-2, Mathayo 17:19-20) na pia kufunga ili kumkaribisha Roho Mtakatifu


MUNGU WANGU AWABARIKI

Comments