MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATARE AWAMBIA WAUMINI WAKE KUWA SOMO LA JUMAPILI NI LAKUKUNJA USO, TOFAUTI NA MASOMO YALIYOPITA
 Mchungaji Getrude Rwakatare
 Waumini
Mchungaji wa Mlima wa Oto Mikocheni B aliwaambia waumini wake kuwa leo wanalishwa ndimu na sio chakula kitamu maana somo la leo litagusa maisha yako kwa kiwango kikubwa. Na somo lilikuwa kama ifutatavyo:
Mchungaji Rwakatare: Bwana Yesu asifiweeeeeee
Waumini: Ameeeeeni 
Mchungaji Rwakatare: Leo nimekuja na uso wa ndimu, nawalisha chakula ambacho hamjawahi kula. Leo tutajifunza

MAOMBI YA VITA
Ufunuo 12:7, Petro 5:8-9)
-Shetani alifukuzwa mbinguni na kutupwa duniani kutokana na uovu wake. Shetani amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa wanadamu kwa kuanzisha vita vya kiroho, na Mungu anasema vita vyetu kama wanadamu si vya kimwili bali ni vya kiroho dhidi ya adui shetani. Hatuwezi kupambana naye kimwili kwasababu hatumuoni.
 
Waimbaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Joy Bringers

Maombi ndio silaha na ni dawa kwa kila amwaminiye BWANA. Kwa kupitia maombi yako kwa Mungu unaweza pia kupambana na shetani. Watu wengi wakati wa maombi wanadharau, utaona wengine wanakosa hata heshima katika kipindi cha maombi, watu wanatafuna bigijii, wanaongeaongea, wanaachama midomo yao kama njaa zinawauma, wanasinzia wakati wenzao wanaendelea na maombi na wengine wanaiga tu wenzao na hawamaanishi kile wanaongea na Mungu wao. Maombi ni ukombozi, unatakiwa kufunga na kuomba.
Wachungaji wetu wanapaswa kukumbushwa wakati wa maombi. Kuna baadhi ya wachungaji hawasisitizii waumini wao kuomba na badala yake wanaweka fedha mbele na kusahau kuwa hizo pesa zinakuja kwa msaada wa maombi.
Watu wamechukulia maombi kama ni kitu cha kawaida, na shetani anapoona huombi anafurahi sana na ni rahisi sana kwake kukuingia kwasababu kunakuwa hakuna kipingamizi chochote ndani yako (huna silaha yoyote ya kumzuia shetani)

 Waumini

(Mathayo 11:12)
Ufalme wa Mungu hukuongezea matumaini. Watu wengi wanafurahia sana kuona maombezi ya Nabii TB Joshua wa Nigeria akiombea watu mbalimbali, lakini cha kujiuliza ni kwamba, unafaidika nini unapoona wengine wanaombewa na wewe umekuwa ni mtazamaji tu? Wengine wanapona na wewe umebaki na ugonjwa wako, wengine wanapata safari za Ulaya wewe bado ukouko tu. Simama kama wewe, omba kwa Mungu wako kwa juhudi zako zote, Na kumbuka huwezi kupokea kwa Mungu kama hujatubu dhambi zako kwanza kabla ya maombi nakusamehe waliokukosea. Mungu huangalia mioyo iliyosafi na sio iliyochafuliwa na maovu.
Huwezi kumshinda sheatani kwa kuimba mapambio tu bila ya kuwa na Mungu ndani yako kwa kupitia Roho Mtakatifu. Pia ka,a ,ao,bi yako ni kilelemama huwezi kufanikiwa, maombi yako yawe na nguvu mbele za Mungu. Hii ninamaanisha ombi kwa kumaanisha na kuwa na imani unahoomba kinatendeka. Ukiwa huna imani na kile unaomba hutafanikiwa na hutapokea chochote.

KWANINI NI LAZIMA KUPAMBANA NA SHETANI?
1/  Kujitetea mwenyewe
-Sheatni hutakutafuta huku na huku ili akumeze (Yakobo 4:7, Yohana 10:16). Shetani huja ili aibe na aharibu kile ulichonacho. Shetani anaweza kumtumia rafiki au ndugu ayko kukuharibia mipango yako, kwahiyo hupaswi kumchukia ndugu yako au rafiki yako aliyekukwaza ila mchukie shatani.
Tenga Muda wa maombi na sehemu ya kufanyia maombi, kama ni chumbani, funga milango yako na aanza maombi.
 Wachawi hutumia ‘REMOTE” zao kuendesha maisha yetu na kfanya vile wanataka kufanya. Tunapaswa kukemea hizo nguvu kwa jina la Yesu Kristo.
Usikubali kudharaulika, kuonewa, kusemwa, kusengenywa, kwa wewe ni motto wa Mungu
2/  Kurejesha kile kilichochukuliwa na shetani
Kama wewe umeibiwa mchumba wako, mume wako, mali zako au unakesi ya kusingiziwa, ukiwa na Mungu na ukamwani na kumtumikia vyema, hivyo vyote vitarudishwa.
Amgali sana watu unaowakopesha wengine huwa hawarudishi pesa baada ya kukopa. Kama utakutana na mwamini wa Mlima wa Moto Mikocheni B amnataka kukukopa pesa zaidi ya 50,000 naomba unitaarifu mchungaji wako na mimi nitakula naye sahani moja.
Mara nyingi shetani anapokuwa ameingia kwako, hapendi kutoka, ni lazima ufanye kazi ya ziada kumuondoa ili baraka zako zirudi. Shetani huzuia barajka zako au mafanikio yako anapokuwa ndani yako
Wachawi lazima wauawe kwani si wazuri katika maisha yako, na mchawi utamuua kwa maombi na sio kwa kutumia silaha za kimwili. Kuna watu wangekuwa mbali katika maisha yao lakini shetani amekalia baraka zao
(Methali 6:31) Mtu anayekuloga anakualibia utukufu wako.
3/ Kujifungua katika kifungu cha shetani
Tunaaswa kufanya maombi ya kutaa kazi za shetani kwa kukata mifungo vyake vyote. Kuna vifungo mbalimbali:-Mafanikio, maendeleo katika maisha yako n.k.
Mungu anataka utoke mahali hapo nauende mahali pengine, na unaweza kutoka kama utakuwa umeweka maisha yako kwa Yesu na kuwa mtu unayefanya kazi za Mungu na kuachana na dhambi. Kusoma Neno la Mungu kila wakati ili kuidumisha imani yako.
Shetani hana raha anapoona wewe unafanikiwa katika maisha yako, anapata taabu sana anapoona unatumia jina la Yesu kwa kuyafanikisha maisha yako.
Kama kanisa lazima tuwe imara na msimamo mkali katika kufanya kazi ya Bwana. Kuna watu wanakarama tofautitofauti ambazo wanaweza kuzitumia kumtangaza Kristo, sio wote lazima kuwa wachungaji, waainjilisti, maaskofu. Unaweza ukawa wewe ni mtoaji au unautalamu Fulani kwa kazi ya Bwana
Usikubali kulindwa na shetani mabaye haonekani kwa macho. Tuwe watu wa maombi sana na watakatifu. Kumbuka maombi ya usiku yana nguvu sana mbele za Mungu.
Ukitaka kujiinua lazima ujitakase nikimaanisha usiwe na doa la dhambi kwa kutubu maovu yako. Unapofanya mabaya unamruhusu shetani kuingia kwako. Dhambi ni chukizo mbele za Mungu.
4/ Ni haki mbele za Mungu kuwalipa wale watutesao, misukosuko na mihangaiko.
(Wathesalonike 2:1)
Ni haki kulipa misukosuko kwa watu wateswao na misukosuko na kuwapa raha. Si haki kwao kuwa na maisha ya kubahatisha.
Watu wanakosa maarifa ya kuwangusha shetani, kwa kutumia jina la Yesu ambalo ni ngome a,bapo watu wenye haki hulikimbilia na kuwa imara
(Wakoritho 2:10:3-6, Methali 18:10, Ufunuo 12:11)
Silaha za Mungu ambazo unaweza kuzitumia ni kama:-
a/ Moto wa Mungu
b/ Damu ya Yesu
c/ Sifa
(Nyakati 2:20)

Comments