KWANINI UTESEKE NA YAESU YUPO KWAAJILI YAKO. USIKOSE IBADA YA KUTENGWA NA GIZA NENE LEO IJUMAA



BWANA APEWE SIFA..!

Leo Ijumaa 11.01.2019 tutakuwa na ibada ya KUTENGWA NA GIZA NENE KATIKA MAISHA YAKO (Mwanzo 1:1) . Ibada itaanza saa 9 alasiri hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" jini dar es Salaam. Jitahidi kupanga muda wako vizuri na hakikisha unakuwepo nyumbani mwa BWANA kwaajili ya faida yako na kizazi chako kwa mwaka 2019. Yawezekana mwaka mzima umekuwa katika giza nene la magonjwa, madeni, kutooa/kuolewa, kutopata watoto, mimba kuharibika, magonjwa, mikosi, kufukuzwa kazi mara kwa mara, kukosa kibali na mambo mengine kama hayo lakini leo AMINI BWANA atafanya kitu katika maisha yako. Kwanza naomba UAMINI, uchukue hatua na ufanye maamuzi magumu ya kuacha hizo shughuli zako na uje hapa kanisani ukutane na huruma za BWANA katika maisha yako. Kuthubutu kwako na kuamini kwako ndio chanzo cha MAFANIKIO yako katika mapito uliyopitia mwaka 2018. Tutakuombea na kumuomba Mungu akusamehe kwa makosa uliyofanya na yakasababisha ukakosa baraka zako kwa mwaka 2018. Tutaomba Mungu afungue njia za mafanikio na maongezeko kwa mwaka 2019


Ubarikiwe na nisaidie sana KU SHARE au Kusambaza tangazo hili. Asante.


-----------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Comments