JE, UNAAMINI LEO NDIO SIKU YAKO YA MUUJIZA WAKO? KAMA UNAAMINI NAOMBA TUKUTANE BAADAE KANISANI.

Mungu akutunze mwanangu. Ijumaa hii ikawe ni ya baraka kwako, kila utakachokifanya kikafanikiwe kwa Jina la Yesu. Mungu akusaidie siku ya leo tukutane kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 9 alasiri kwaajili ya kufanya maombi maalum ya KUTENGUA GIZA nene lilokuziba usione mafanikio yako ya mwaka 2018. Tutamuomba Mungu akupe NURU kwaajili ya kupokea baraka zako ulizozikosa mwaka 2018. Mwaka huu ukawe ni mwaka wako wa ONGEZEKO na MAFANIKIO kwa kila jambo unalolifanya. Ibada itaanza saa 9 alasiri. Hebu jaribu kuacha hizo kazi zako ili Mungu azidi kukupa akili na maarifa katika kazi zako za mwaka 2019. Mimi nipo mlangoni nakusubiri pamoja na watumishi wa Mungu wa hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tutafurahi sana kukuona kanisani ukiwa na waumini wenzako mkisubiria miujiza kutoka kwa Mungu mwenyewe. MWANZO 1:1. Nakupenda sana mwanangu.


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni "B"


Comments