31.12.2019: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA




Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona tena tarehe yangu ya kuzaliwa kwangu ambayo ni tarehe 31.Desemba. Mungu amekuwa mwema kwangu kwa kunipa kibali cha kushuhudia tena tarehe yangu ya kuzaliwa. Nina kila sababu ya kukushukuru wewe ambaye ulikuwa ukiniombea na hatimaye leo nimeona matunda ya maombi yako ya kuwe kuiona tena siku yangu ya kuzaliwa. 




Napenda kuishukuru kamati ya maandalzi ya sikuku ya kusherekea kuzaliwa kwangu. Hakika nimeona juhudi zenu na mapenzi mema kwangu. Mmeona ni vyema mkafurahi na mtumishi wa Mungu na mmekuwa mstari wa mbele ya kuniombea ili nisonge mbele na kazi ya Mungu.


Pia napenda kuwashukuru watu wote waliojinyima na kuweza kuniandalia cake nzuri. Mungu awabariki sana, mwaka 2019 ukawe ni mwaka wa mafanikio na maongezeko katika maisha yenu. Kila utakachokifanya kikafanikiwe kwa jina la Yesu. Mungu akaweke ulinzi katika kazi za mikono yako.


Nawapenda watu wote mliofika na kuwezesha shughuli hii ya kusherekea siku yangu ya kuzaliwa ambayo imefanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mungu niliyemtumikia kwa zaidi ya mika 40 ya wokovu wangu asiwaache peke yenu bali awe nanyi katika shughuli zenu za kila siku. Kila mtakalolifanya kwa mikono yenu likafanikiwe na kuongezeka. Mungu akawaepushe na mabaya na mipango ya shetani. Nenda ukang'are mwaka 2019...Amen.

-----------------------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Mlima wa Moto Mikocheni "B"

















































































Comments