13.01.2019: MUUMINI AMSHUKURU MUNGU KWA KUMVUSHA SALAMA KATIKA MAPITO ALIYOPITIA KATIKA FAMILIA YAKE.





Muumini na mhudumu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 13.01.2019 kwenye ibada ya Kurejesha Shehena ya Ajira, Biashara, Kazi, Afya Njema, Mahusiano n.k iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kumshukuru Mungu katika mapito aliyopitia katika familia yake na jinsi Mungu alivyomsaidia kuvuka salama. Alimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, wazee wa kanisa, vijana, waumini waliomtia moyo na kumuombea katika kipindi cha mapito yake. Pia aliwaomba waumini wa kanisa hilo wajiunge na vikundi vilivyomo ndani ya kanisa ili kuwe na wepesi wa kujua shida ya mtu na kuweza kumsaidia kwa wakati sahihi. 

Mungu wetu anatuagiza ya kuwa "Lia na wanalio, furahi na wanaofurahi na huo ndio upendo." 

Mungu akubariki na tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3



















Comments