13.01.2019: DADA ATOA KITENGE KWAAJILI YA KUCHANGIA MAENDELE YA KANISA.

Bwana Apewe sifa. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kitendo alichomfanyia huyu dada aliyeamua kutoa sadaka yake ya kitenge ili kiuzwe madhabahuni na pesa itakayotikana iwe ni kwaajili ya maendeleo ya kanisa. Dada huyu ambaye ni mfanyabiashara wa vitenge aliamua kufanya haya yote siku ya Jumapili 13.01.2019 katika Kongamano la Siku Moja la Kurejesha Shehena ya Utajiri, ajira, kazi na kila kitu ulichopoteza. Kongamano hili lilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunamshukuru Mungu kwa kumpa maono hayo na kuonyesha upendo wake kwa kanisa analosali na jinsi anavyompenda Mungu wake aliyemuumba.

Mzee wa kanisa Mzee Malya akikitangaza kitenge











Comments