06.01.2019 | WACHUNGAJI NA WATOTO WADOGO WAPAKWA MAFUTA YA UPAKO

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 06.01.2019 kwenye ibada ya Kupeleka Mahitaji Yetu ya Mwaka 2019 kwa Mungu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", waliweza kuwaombea watoto wadogo ili Mungu aweze kuwalinda katika masomo yao, afya zao, michezo yao ya utotoni na shughuli zao mbalimbali wanazofanya mashuleni kwao au majumbani kwao. Ila kubwa zaidi niu kuwataka watoto hawa wakue katika kumpendeza Mungu na kuishi maisha matakatifu. Baada ya maombezi Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwapaka mafuta ya upako wachungaji watakaowapaka mafuta watoto wadogo na baadae wachungaji waliweza kuwapaka mafuta ya upako kwa kila mtoto aliyefika kanisani. Mungu awabariki wazazi au walezi kwa kuwaruhusu watoto kuja kanisani ili wakutane na Mungu katika maisha yao. Tunategemea sasa wazazi wataongeza juhudi za kuwaombea watoto wao na kuwafundisha njia sahihi ya kumtumikia Mungu wakiwa bado wadogo na hata watakapokuwa watu wazima. Watumishi wa Mungu wako mstari wa mbele kuwaombea watoto hawa na kuwafundisha Neno la Mungu kila Jumapili katika madarasa yao ya Sunday Scholl hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Yesu aliwapenda watoto wadogo nasi tuwapende watoto wadogo. Mungu awabarikisana.




Mch. Sylvanus Komba akipakwa mafuta 









































Comments