06.01.2019: MCH. SYLVANUS KOMBA AFANYIKA BARAKA KATIKA IBADA YA KUPELEKA YA MWAKA 2019 MAHITAJI YETU KWA MUNGU.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mambo makubwa aliyoyafanya siku ya Jumapili 05.01.2019 kwenye ibada ya Kupeleka Mahitaji Yetu Kwa Mungu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mtumishi wa Mungu Mch. Sylvanus Komba kutoka kanisa la Mlima wa Moto Dodoma alitubariki sana kupitia mahubiri yake aliyohubiri katika hekalu la Mungu la Mlima wa Motop Mikocheni "B". Ujumbe wake ulikuwa ni wa kutuelimisha, kutuadibisha na kutufundisha njia sahihi ya kwenda mbinguni kwa Baba na hasa kutukumbusha kutenda mema na kuacha maovu. 

Tukiwa katika maandalizi ya kukuletea mahubiri yake hebu angalia matukio kwa njia ya picha yaliyotokea wakati akihubiri hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". 

Na Jumatatu hii usikose kushiriki ibada ya Kuvunja laana na maneno mabaya uliyotamkiwa na ndugu zako na marafiki zako au na watu usiowajua kutoka kijijini kwako ambao wamekunenea maneno ya kukuangamiza kiafya na kiuchumi ili usifikie malengo yako ya mwaka 2019. Njoo na leso/ kitambaa chako cheupe kikiwa kimeandika jina la Kijiji chako au karatasi nyeupe ikiwa imeandikwa jina la kijiji vchako. Usipange kukosa ibada na mamombezi yataanza saa 9 alasiri

----------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Mlima wa Moto Mikocheni "B"





























Comments